![]() |
| Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Rodrick Mpogolo |
Na Mwandishi wetu KTPC,Katavi.
Uzalishaji wa zao la Pamba katika Mkoa wa Katavi bado uko chini hali iliyopelekea mwekezaji wa kiwanda cha pamba kubadili matumizi ya fedha za kununulia zao hilo kwa kuzielekeza kwenye kununua zao la mahidi.
![]() |
| Balozi wa Pa,mba nchini Aggrey Mwanri. |
Kwa takwimu uzalishaji wa zao la pamba katika Mkoa wa Katavi kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2020/21 ni kg 2,173,399 zimezalishwa na kufanya kiasi hicho kuwa ni kidogo hasa ukizingatia soko la zao hilo liko wazi kupiti mwekezaji wa NGS Investment Co Ltd kilichopo wilaya ya Tanganyika kikiwa na uhitaji wa kg Mil 50 wa zao hilo.
Katibu Tawala
wa Mkoa wa Katavi,Rodrick Mpogolo kwa niamba ya Mkuu wa Mkoa Mwanamvua Mrindoko
amesema hayo jana katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani hapa wakati wa
kufungua kikao cha wadau wa kilimo cha pamba kilicholenga kutoa hamasa na elimu
ya kuzingatia uzalishaji wenye tija uliotolewa na bodi ya pamba Tanzania.
Mpogolo amesema
kuwa msimu wa maadalizi wa kilimo cha pamba umeanza na zoezi la uhamasishaji wa
kutoa elimu kwa mkulima ni muhimu kwa Mkoa kutokana na uzalishaji wa zao hilo
kuwa chini kwa kuzingatia takwimu za kg
zaidi ya mil 2 ikiwa ni hasi ya kama Kg mil 47 hadi Kg Mil 48.Ikiwa sawa na
kupewa fedha ziko na kushindwa kuzichukua.
![]() |
| Balozi wa pamba nchini,Aggrey Mwanri wakionesha namna ya kupalilia kwa ufanisi ili kuchochea ufanisi |
“ nitoe tu kwa wasitani kama kg 1 ya pamba inauzwa kwa Tsh 1,000/- ukizidisha mara Kg mil 50 ni sawa sawa na bilioni 50 ambazo zinaingia kwenye mkoa wetu,lakini sisi hatujawaada wakulima kuchukua hizo billion 50” Alisema Katibu Tawala.
Amefafanua mkoa bado unatatizo na kinachotakiwa kufanywa na watalamu,bodi ya pamba Tanzania na mwekezaji kuwaunganisha wakulima waingie kwenye kilimo cha pamba cha kisayasi ili wazichukue hizo fedha ziingie katika mifuko yao na kuboresha kipato cha familia na mkoa wa Katavi.
Mpogoli amesema
“ nilipata kutembelea kile kiwanda cha NGS,Meneja akaniambia kuwa anazo pesa
benki kwa ajili ya kupeleka kwa wakulima
lakini kwa kuwa hakuna pamba sasa amelazimika kuanza kuchukua mahidi…sasa baada
ya kukosa anachukua mahidi ya wakulima kitu ambacho hakikupangwa kwa ajili ya
mahidi”.
Aidha licha
ya kuushukuru wijio wa bodi ya pamba Tanzania kupitia balozi wake Aggrey Mwanri
na watalaamu wengine amesema kwenye utekelezaji wa malengo ya kilimo
wamefanikiwa kugawa mbegu za pamba kwa msimu mpya wa kilimo wa mwaka 2021/22
na kutoa wito kwa wataalamu wa sekta
hiyo kuingia shambani na kuacha kukaa ofisini na kupunguza kuandika na kwenda
kufanya kazi kwa wakulima.
Renatus Luneja,Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya pamba Tanzania amesema kapeni hiyo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yam waka 2020/25 inawataka kuzalisha tani milioni moja za pamba ifikapo mwaka 2025.ili kufikia malengo hayo wameweka mikakati ya kuhamasisha wakulima kuongeza tija kwenye uzalishaji wa zao la pamba.
Ameeleza kuwa
sehemu nyingi wakulima huzalisha wastani wa kg 300 za pamba kwa hekali moja
ikiwa afadhari kwa mkoa wa Katavi huzalisha wastani wa kg 500 za pamba kwa
hekali moja.Hivyo uwezo wa mbegu kwa mujibu wa tafiti angalau wasitani wa kg
1,000 zinatakiwa kuzalishwa kwa hekali moja na kusaidia kufikia malengo ya tani
milioni moja kitaifa
“ Katavi ni eneo la kimkakati tutakuwepo kwa siku 14 kutoa elimu,Na kwa mkoa huu mmewekewa malengo ya kuzalisha tani 50,000 za pamba kwa mgawanyo wa tani 25,000 halmashauri ya wilaya ya Tanganyika,Tani 16,000 halmashauri ya Nsimbo,Tani 4,000 halmashauri ya wilaya ya Mlele,Tani 5,000 halmashauri 5,000 manispaa ya Mpanda” alisema Lunneja..
Balozi wa zao
la pamba Tanzania,Aggrey Mwanri amesema kuwa pamba ni zao muhimu la biashara
ambalo linaliingizia taifa fedha za kigeni na wameendelea kufanya kampeni
katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Simiyu,Geita,Mara na Tabora ambapo wamekuwa
wakiwahimiza wakulima kufanya kilimo cha kisayansi.
Mwanri amefafanua
kuwa katika utoaji wa elimu wamekuwa wakihimiza utayarishaji mapema wa
shamba,kutumia mborea za samadi na virutubisho vingine,kupanda pamba
mapema,kupanda kwa mistariii na kwa nafasi maalum,kupanda idadiiii halisi ya
mbegu katika kila shimo,Kupunguza miche na kupalilia kwa wakati.
Mambo mengine ni kunyunyuzia madawa kuzuia wadudu waharibifu kwa kuzingatia athari za kutokunyunyuzia,kuvuna pamba mapema na kuchambua pamoja na kung’oa na kuchoma moto masalia yote ya pamba.


