![]() |
| Maria Salvatory,Fundi wa vifaa vya umeme akitengeneza moja ya spika ya radio iliyoharibika. |
Na Irene Temu,Mpanda.
Katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi, Maria Salvatory (25) mwanamke kijana amekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa manispaa hiyo kutokana na umahili wake wa kutengeneza vifaa vya umeme kama vile radio na simu za mkononi.
Akizungumza na blog hii leo ofisini kwake iliyopo mtaa wa Fisi,Kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda Mkoani hapa,Maria Salvatory ameeleza kuwa tangu akiwa mtoto mdogo wa umri wa miaka 15 alivutiwa zaidi na kazi ya ufudi wa vifaa vya umeme kutokana na kuwa mjomba wake Alex Thomas kwa muda mrefu amekuwa akifanya kazi hiyo.
“…nikiwa na umri mdogo nilikuwa mtundu sana mara nyingi nilipigwa viboko na Baba yangu kwa sababu mara nyingi nilikuwa nikichokonoa radio ya nyumba na mara kadhaa kuharibu kabisa” Amesema Maria ambapo amesisitiza kuwa hakuweza kukataa tamaa ya kujifunza zaidi licha ya kuadhibiwa.
Maria amesema kuwa baada ya kumaliza elimu ya sekondari mwaka 2015 hakuweza kufaulu na kuendelea na masomo ya kidato cha tano,ndipo muda mwingi aliuwekeza kweye kujifunza zaidi masuala ya ufudi licha ya kuwa wanaume wengi walishindwa kumwelewa.
“Ni kweli watu wananikodolea macho…ninapotengeneza simu huwezi kuamini wakati mwingine utakuta vijana wengi wamenizonga hapa ofisini.Wapo wenyenia ya kunipima kama ninauwezo huo wa kutengeneza simu na wengine hutazama kwa kutokuamini,inawezekanaje kuwa mwanamke ninayetengeneza simu” Amesema Maria.
Ameeleza kuwa hapo awali alikabiliwa na changamoto nyingi kama vile jamii kutokumbali na kumwona sio mtu mwenye maadili mema kutokana na jamii kuamini kuwa mwanamke yafaa zaidi kufanya kazi za nyumbani kama vile kupika chakula.
“…hali kwa sasa imebadilika lazima niwe mkweli mimi ni mama wa mtoto moja na kazi hii inanisaidia pakubwa kukidhi gharama za maisha kwa sababu mwenza wangu sio mtu wa kujali sana familia” Amesema Maria huku akitabasamu.
Mrisho Juma,Mkazi wa mtaa wa Nsemlwa Manispaa ya Mpanda ambaye radio yake imetengenezwa na fundi huyo amesema kuwa ni jambo la vijana wa kiume wanapaswa kumtia moyo Maria kwani anaonesha wazi kuwa dhana ya mwanamke ni mtu wa kuelea watoto pekee imeshapitwa na wakati.
Amesema kuwa kama vijana wa kiume wanapaswa kuwaruhusu wake zao kufanya kazi hasa ambazo jamii imekuwa ikiziona niza mwaume pekee.
Loveness Jackson,Msichana wa kidato cha tatu katika sekondari ya Mwangaza Manispaa ya Mpanda asema kuwa fudi Maria amekuwa kivutio kikubwa kwake binafsi na kumsukuma kutia juhudi kwenye masomo yake kwani anadoto ya kuwa mwandisi msanifu wa majengo.
