| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad |
Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Lucia Chaya (15) Mkazi wa Kijiji cha Tumaini Kata ya Itenka Wilaya ya Mpanda amefariki Dunia hapo hapo baada ya kupigwa na radi wakati akiwa chumbani kwake na mtu mwingine mmoja amejeruhiwa waliyekuwa wakiishi nae kwenye nyumba moja .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi All Makame Hamad amewaambia Waandishi wa habari kuwa tukio hili limetokea hapo juzi majira ya saa kumi na mbili jioni huko katika Kijiji cha Tumaini Kata ya Itenka Wilaya ya Mapanda .
Kamanda Hamad amesema marehemu huyo alipigwa na radi na kufariki dunia hapo hapo wakati akiwa amelala chumbani kwake na kumjeruhi mtu mmoja aliyekuwa akiishi naye ndani ya Nyumba hiyo.
Alifafanua kuwa kufuatia mvua nyingi zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi huku zikiwa zimeambatana na upepo mkali ndio chanzo Cha kifo hicho.
"nikwamba katika tukio hilo mtu mmoja pia amejeruhiwa kwa kupigwa na radi ambae anafahamika kwa jina la Anna John(38) Mkazi wa Kijiji cha Tumaini Kata ya Itenka ambaye walikuwa wamepanga nyumba moja na marehemu huyo lakini wakiishi kwenye vyumba tofauti.
Kamanda All Hamad amesema kuwa mara baada ya tukio hilo Anna John alikimbizwa katika zahanati ya Itenka kwa ajili ya kupatiwa matibabu na hali yake kwa sasa inaendelea vizuri.
Katika tukio lingine huko katika Kitongoji cha Moto moto Kijiji cha Mapili Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele mvua kubwa iliyonyesha na kuambatana na radi imepiga nyumba mbili za familia moja ya Kisinza Saluhe (93) .
Kamanda Hamad amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa mbili na nusu usiku ambapo katika tukio hili hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyotokea isipokuwa mali iliyokuwemo ndani na vyombo pamoja na nguo zimeteketea kwa moto uliosababishwa na radi hiyo .
Amebainisha kuwa thamani ya vitu hivyo vilivyoteketea vya kikongwe huyo vina thamani ya shilingi laki saba na nusu.