Yusuph Mahundi Meneja Mahusino na usimamizi wa Kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA akimkabidhi kadi ya Pikipiki Mkuu wa kituo cha Polisi mishamo. |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Kampuni ya
ununuzi wa Tumbaku ya
PREMIUM ACTIVE TANZANIA imetoa
msaada wa usafiri
wa Pikipiki kwa kituo cha Polisi
cha Mishamo katika Mkazi ya wakimbizi
Mishamo Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi utakaosaidia shughuli mbambali
za kuimarisha usalama kwenye eneo hilo.
Mkuu wa kituo cha Polisi Mishamo Andrea Msesemi kushoto akitoa shukrani zake kwa kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA kwa kuwapatia usafiri wa Pikipiki. |
Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA imetoa msaada wa usafiri wa Pikipiki kwa kituo cha Polisi cha Mishamo katika Mkazi ya wakimbizi Mishamo Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi utakaosaidia shughuli mbambali za kuimarisha usalama kwenye eneo hilo.
Msaada huo wa pikipiki ya kisasa yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni nne umekabidhiwa na Meneja uhusiano na usimamizi wa Kampuni ya Premium Tanzania aliyekabidhi kwa niaba ya Kampuni hiyo .
Mahundi akikabidhi pikipiki hiyo yenye ukumbwa wa CC 250 amesema wao kama kampuni ya Premium walipokea ombi kutoka Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi kwa ajiri ya kituo cha polisi cha mishamo .
Kuitokana na ushirikiano ambao wamekuwa wakiupata katika shughuli zao za ununuzi wa Tumbaku kwenye eneo hilo na kwa Mkoa wa Katavi kutoka kwa wadau mbalimbali na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi.
Hivyo waliona ni jambo njema sana wao kama kampuni ya Premium Active Tanzania kuweza kusaidia kwenye swala la usafiri ambao utasaidia kuwezesha swala la usafiri kwa kituo cha Polisi Mishamo .
Mwakilishi wa Mkuu wa Makazi ya Mishamo Jimmy Molle amesema wao kama ofisi ya Mkuu wa Makazi ya wakimbizi ya Mishamo wamefurahi sana kuona kituo cha Polisi kinakabidhi wa usafiri wa pokipiki ya kisasa na imeonyesha jinsi ambavyo kampuni ya Premiun inavyo wajari na inavyorudisha fadhila kwenye jamii.
Amebainisha kuwa kituo hicho cha Polisi kulikuwa na changamoto kwani usafiri wao ulikuwa umechakaa hivyo pikipiki hiyo itasaidia sana kuimalisha usalama kwenye maeneo yao kwa kuhakikisha yanakuwa salama zaidi .
Molle ameeleza kuwa pia itasaidia wadau wao hasa wakulima wa Tumbaku kuzuia baadhi ya wakulima ambao walikuwa sio waaminifu kwa kutorosha tumbaku kwenda sehemu nyingine kwa lengo la kukwepa deni la pembejeo .
Mkuu wa Kituo cha Polisi Mishamo Andrea Msesemi amesema anatoa shukurani za dhati kwa Kampuni ya Premium kwa msaada huo muhimu kwa Jeshi la polisi kwa kuweza kukubali kupokea maombi yao .
Amesema wao kama polisi wataendelea kuwatambua kampuni hiyo kama wadau wao mhimu ambao wameweza kuwapatia chombo cha usafiri kwa jeshi la polisi Mishamo itakayo wasaidia kuweza kupambana na uhalifu na wahalifu .
Amefafanua kuwa kwani itawasaidia kwenye dolia zao wanazofanya kila siku kutoka kijiji kimoja kwenda kijiji kimgine kutoka na eneo hilo la ,makazi kuwa na eneo kubwa hivyo itawasaidia sana .
Amesema kwa ujumla anaishukuru kampuni ya Premium kwa Msaada huo huku akiiomba kampuni hiyo kuendelea kuwa wadau mhimu wa ulinzi na usalama kwa kutoa pikipiki ili kuimarisha ulinzi wa Raia na Mali zao.