HAKUNA KIUNGO CHA SIRI KINACHOONDOLEWA BAADA YA KUTEKELEZA MAUAJI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad akionyesha Waandishi wa Habari baadhi ya silaha aina ya Gobore,shoka,kisu na gololi za Chuma wanazotumia wahalifu kuwinda wanyama ndani ya Hifadhi ya Taifa ya wanyama pori Katavi

Na Irene Temu
Katavi

Wakazi wa Manispaa ya Mpanda wameondolewa hofu na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Juu ya matukio ya mauaji yanayotokea ndani ya Mkoa wauaji kuchukua sehemu za Siri baada ya kutekeleza mauaji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad ameeleza hayo mbele ya Waandishi wa Habari ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya matukio mbalimbali yaliyoripotiwa kutokea ndani ya Mkoa wa Katavi.

Nakusema kuwa mnamo tarehe 2, April 2022 katika mtaa wa Ilembo Tarafa ya Misunkumilo Wilaya ya Mpanda Stamiliya Hussein(27) muuza duka la madawa ya binadamu aliuwawa kwa kupigwa na kitu kizito chenye ncha Kali maeneo ya kichwani na kufariki papo hapo.

Baada ya mauaji hayo Wananchi wa Manispaa ya Mpanda walizua taharuki juu ya mauaji hayo kuwa watekelezaji wa mauaji wanachukua sehemu za Siri baada ya kutekeleza mauaji.

Hivyo Kamanda Hamad amewatoa hofu Wananchi wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla hakuna mwili wowote uliokutwa umeondolewa viungo vya Siri vya mwili baada ya kuuwawa.

Kwa upande mwingine Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kutoka Mkoa wa Tabora  waliokodiwa kwa lengo la kutekeleza  mauaji ndani ya Mkoa wa Katavi.

Watu hao walipanga njama za kumuuwa Krasii Nyagwida(30) Mganga wa kienyeji Mkazi wa Inyonga Mkoa wa Katavi baada ya kukodiwa na mke wake Gwere Nyadwida(25)  kwenda kumuuwa mume wake kwa chuki kuwa anamzidi nguvu katika shughuli za uganga wa kienyeji.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi lilifanikiwa kuzuia jaribio hilo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watatu ambao ni Yahaya Kasimu(28)fundi rangi,Oscar Charles (39) na Emanuel Mushona(34) waliopanga kutekeleza mauaji hayo Mach 23,2022 nyakati za usiku ndani ya Mkoa wa Katavi.

Baada ya watuhumiwa hao kukamatwa na Jeshi  la Polisi Mkoa wa Katavi wakiwa bado Mkoa wa Tabora hawajafika Inyonga Mkoa wa Katavi kutekeleza mauaji wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na Upelelezi utakapokamilika watafikishwa Mahakama kujibu tuhuma zinazowakabili.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages