![]() |
Walengwa waliopo katika Mpango wa kunusuru Kaya maskini kutoka TASAF wakijishughulisha na biashara kupitia ruzuku wanazopokea kutoka TASAF ili kujikwamua katika Hali duni ya umaskini waliyopo. |
Na Irene Temu
Mpango wa kunusuru Kaya za Walengwa kupitia TASAF umekuwa mkombozi kwa kaya zilizokuwa zikiishi katika hali duni baada ya kuingia katika Mpango huo na kuhawilishiwa fedha.
Uhawilishwaji huo unaofanywa na TASAF kwa kuwapatia kiasi Cha fedha kwa Kaya za Walengwa umesaidia kaya hizo kuondoka na umaskini waliokuwa nao na kubadili maisha yao.
Katika kudhibitisha hilo Walengwa wa kaya maskini zinazohawilishwa fedha na Mpango huo katika Vijiji vya Kumbanga na Kumhasha vilivyopo katika Kata ya Mlungu Halmashauri ya Wilaya Kibondo mkoani Kigoma wamebainisha kuwa maisha yao kubadilika.
Miongoni mwa walengwa walionufaika na Mpango huo wa kunusuru Kaya za Walengwa ni kijana Shukuru Aloyce anayeshuhudia mafaniko aliyo nayo kutokana na Mpango huo.
Shukuru anasema Wazazi wake walikuwa miongoni mwa wanufaika wa Mpango, na baada ya Wazazi wote wawili kufariki aliteuliwa kuendelea kupokea ruzuku hiyo ambayo aliitumia kulea wadogo zake kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mkubwa na msimamizi wa Kaya.
"nilikuwa nikipokea fedha kutoka TASAF kidogo nilizitumia kwa matumizi ya nyumbani na wadogo zangu"
"Mwaka jana, TASAF walikuja na Mpango wa kusaidia Vijana waliokwama kuendelea na masomo *(Vijana Salama)* walitupatia mafunzo ya siku saba na baadae walitupatia fedha shilingi laki moja na elfu sabini (170,000/-) nilianzisha Biashara ya kuuza maandazi na na vyombo vya nyumbani vilivyokuwa na mtaji wa shilingi elfu themanini (80,000/-) na shilingi elfu tisini nilinunua migomba na kuipanda kwa ajili ya biashara na matumizi ya nyumbani, faida niliyopata katika biashara ya umachinga nimenunua tripu moja ya mawe natarajia kujenga nyumba." Alisisutiza Shukuru
Pia hakusita kuishukuru TASAF imebadilisha maisha yake na familia yake kutoka hali duni aliyokuwa nayo hadi hapo aliposasa angalau anaunafuu wa maisha na kuahidi kupambana hadi tone la mwisho ili aondokane na umaskini.
"mimi binafsi naumia Sana ninapo sikia neno maskini hivyo kupitia ruzuku hii ninayopokea kutoka TASAF naimani nitaitumia vizuri mpaka niondokane na umaskini" alieleza Shukuru
Nae Mzee William Selele anashuhudia ruzuku waliyokuwa wakiipata yeye pamoja na mke wake waliitumia pia kusomesha watoto wao Shule na sasa kijana wake yupo Chuo Kikuu Dodoma akisoma kozi ya Ualimu na anaimani pindi atakapohitimu masomo yake atakuwa msaada mkubwa katika kuinua maisha ya Kaya yao kwa ujumla.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji Cha Kumbanga Zabron Bangaya ameupongeza Mpango wa kunusuru Kaya maskini kutoka TASAF nakusema awali hali ya umaskini ilikuwa ya kutisha katika Kijiji hicho lakini baada ya kaya maskini kuanza kupokea ruzuku kutoka TASAF hali imebadilika katika kaya hizo.
Bangaya alisema pia watoto wanaosomeshwa na wazazi waliopo katika Mpango wa kunusuru Kaya maskini wanapohitimu masomo yao na kupata kazi wasitelekeze Kaya zao hasa Wazazi waliowasomesha.