MBUNGE KAPUFI AUPIGA MWINGI MIUNDOMBINU YA BARABARA ZA MITAA KWA WANANCHI WA JIMBO LAKE


Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Mtemi  Beda Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda  akiangalia moja ya barabara inayoendelea kukarabatiwa kwenye Mtaa huo  kwa ghrama binafsi za Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini  Sebastian Kapufi.(Picha na Walter MguIuchuma)


Na Walter MguIuchuma

Wananchi wa kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamepongeza hatua ya Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi kuzikarabati Barabara za Mitaa katika maeneo ya Mtaa wa Mtemi Beda  ambao walikuwa na changamoto ya kutokuwa na  miundo mbinu ya uhakika ya barabara.

Akizungumza mmoja wa wakazi wa mtaa huo Janeth Clisensi wakati akishuhudia matengenezo ya barabara hiyo amesema walipokuwa wakipata wagojwa ilikuwa ngumu kuwasafirisha wagojwa hao kutokana na ubovu wa barabara.

".... kutokana na uamuzi wa Mbunge wa Jimbo  letu Mh.Kapufu kuamua kututengenezea barabara hizi za mitaa kwa gharama zake mwenyewe tunamshukuru  kwa jitihada  zake hizo binafsi kwa kuwa magari sasa yatafika, pikipiki na bajaji hivyo usumbufu hautakuwepo tena"alisema Janeth

Nae Laurenti Kitene Mkazi wa mtaa wa Mtemi Beda katika kata ya Misunkumilo  amemshukuru Mbunge Sebastiani Kapufi kwa kufanya kazi zinazoonekana kwa wanachi hasa wananchi wa ngazi za chini kwa kuja na Mtambo wa kukwangua barabara zao kwani zilikua hazipitiki kwa muda sasa na kumuomba  asichoke kuwatumikia wananchi wake kwa vitendo.

Kwa upande wake Firbert Japhet  mkazi wa Mtaa huo naye amesema kuwa barabara hiyo ilikuwa mbovu na mashimo mengi wanamshukuru Mbunge  amewasaidia kutatua kero yao ya muda mrefu na aendelee kuwasaidi katika mambo mengine kama vile Afya,Elimu nk.alisisitiza bwana Firbert.

Katika hatua nyingine Pensi Wiliamu mkazi wa eneo hilo pia la Misunkumilo amesema walikuwa wanapata shida ya kupita na usafiri kama magari na pikipiki na tangu awe mkazi wa eneo hilo hajawahi kuona barabara ya Mtaa inatengenezwa,kitendo cha Mbunge Kapufi kuanza na huo mpango wa kukwangua barabara za mitaani utawasidia Wananchi.

Diwani wa kata ya Misunkumilo Matondo Kanyepo amebainisha kuwa hatua ya Mbunge huyo kuamua kutafuta mtambo kwa fedha yake kwa ajili ya kukarabati barabara kwa kuanza na Kata ya Misunkumilo eneo la Mtemi Beda amezingatia uhitaji na idadi ya watu waliopo kwenye eneo hilo kwani lina idadi kubwa ya wananchi na amemshukuru Mbunge Kapufi kwa kuwatumikia wananchi kwa Vitendo.

Nae Lazaro Sabas Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini ameeleza kuwa tangu mwaka Jana Mh Mbunge akiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani alisema ataanza kuzikarabati barabara zote za mitaa ambazo hazipitiki kwa kutumia Rasilimali zake na alianza kazi hiyo katika kata ya Nsemlwa na Kawajense mwishoni  mwa  mwaka jana.


Barabara ya Mtaa wa Mtemi Beda kata  ya Misunkumilo  Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi

Amesisitiza kuwa zoezi hilo limeanza katika kata ya Misunkumilo na litaendelea katika kata za shanwe na  Kata nyingine zilizopo katika Jimbo hilo la Mpada Mjini pamoja na maeneo mengine ya Manispaa ya Mpanda na kuwaomba wananchi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwa kuwa Mbunge wao yupo nao katika shughuli za maendeleo alisema Lazaro Katibu kutoka ofisi ya Mbunge Jimbo la Mpanda Mjini.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages