PINDA AWAASA WANANCHI WA MIKOA YA MAGHARIBI KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI NYUKI.


Waziri  Mkuu  Mstaafu Mizengo Pinda akiwahutubia wakazi wa Mkoa wa Katavi kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya nyuki Dunia  Kitaifa May 21,2022 yaliyofanyika  Mkoani Katavi katika uwanja wa michezo wa Azimio  ambapo ametoa wito kwa wananchi wa Mikoa ya Katavi ,  Tabora ,Kigoma,  Rukwa na Songwe  kuchangamkia fursa za ufugaji nyuki  ili kuweza kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.(Picha na Walter MguIuchuma)


Walter MguIuchuma

 Katavi

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Peter Pinda ametoa wito kwa wananchi  wa  Mikoa ya Katavi, Tabora  Kigoma Songwe na Rukwa kuchangamkia Fursa ya ufugaji nyuki ili kukuza Uchumi na pato la mwananchi mmoja mmoja.

Kauli hiyo ameitowa wakati  wa  kilele cha siku ya Nyuki Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Mkoa wa Katavi na kusema kuwa Mikoa hiyo ina hali ya hewa nzuri Misitu ya kutosha pamoja na Utunzaji Mzuri wa mazingira.

Amesisitiza kuwa katika kuhakikisha athima hiyo inafikiwa lazima serikali katika Mikoa hiyo ijipange vilivyo hasa kwa kundi la vijana kuendelea kulipatia elimu na uwezeshaji ili wajikite katika ufugaji wa Nyuki kwa kuwa bado fursa hiyo inasoko kubwa na linalohitajika Duniani kwa sasa.

Pinda ameeleza kuwa juhudi hizo ni vyema zikaenda sambamba na Juhudi za kutunza mazingira hali ambayo inaonekana kuwa changamoto kwa baadhi ya maeneo na kupelekea uzalishaji wa Asali kupitia Mdudu Nyuki kufifia kutokana na tatizo la uharibifu wa mazingira.

Katika hatua nyingine Pinda ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuona umuhumu wa kutenga siku ya kuadhimisha siku ya nyuki kwa lengo la kutoa ujumbe kwa jamii juu ya umuhimu wa Mdudu nyuki na mazao ya Nyuki namna ambayo yanaweza kuwa mkombozi wa uchumi kwa wananchi.

Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema Tanzania bado haijafanya vizuri sana katika ufugaji wa Nyuki licha ya Fursa nyingi zilizopo ikiwemo mistu Mikubwa,Mvua za kutosha,maziwa na mito isiyokauka  karibu kila kona amesema sasa umefika wakati wa kubadilika.

" ... Ethiopia ni nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa asali katika bara la Afrika pamoja na kuwa na hali ya jagwa wakati sisi hali yetu ya mazingira  ni bora kuliko ya nchi hiyo hivyo tunahitaji kuongeza utaalamu zaidi katika ufugaji wa nyuki"alibainisha Pinda

Awali akitoa salamu za Mkoa kwa wanachi waliohudhuria hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema pamoja na changamoto zinazojitokeza katika ufugaji wa nyuki katika Mkoa wa Katavi kuna ongezeko la Asilimia 67 la vikunndi vya ufugaji nyuki katika Mkoa pamoja na ongezeko la uzalishaji wa asali na Nta kwa asilimia 23.5.

Ameeleza kuwa kwa sasa kuna ongezeko kubwa kwa wafugaji wa nyuki kuanza kutumia mizinga ya kisasa kwa sailimia 70 hali ambayo inaonekana kukua kwa kasi huku Mapato ndani ya Mkoa yanayotokana na mazao ya nyuki kufikia bilion 13.4 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Mrindoko amesema pamoja na fursa hizo kuwepo katika Mkoa  wa katavi bado kuna mwamkoa Mdogo kwa wanachi kufanya shughuli za ufugaji nyuki hali ambayo inaashiria Elimu kuendelea kutolewa zaidi kwa wananchi kuhusu ufugaji wa nyuki.

Amesisitiza kuwa serikali ya Mkoa wa Katavi inayo Mipango mikakati ya kuendeleza zao la Nyuki na mikakati hiyo imeanza kwa vitendo kwa kujenga kiwanda cha kuchakata Asali kilichopo Wilaya ya Mlele na pia wamejiwekea kuongeza kiwanda kingine ndani ya mwaka mmoja ikiwa ni sehemu ya kukuza sekta ya nyuki katika Mkoa wa Katavi.

Nae Mkurugenzi wa Nyuki Tanzania Dk Ezekiel Mwakalukwa alisema kuwa Maadhimisho  hayo yameenda sambamba na kuzinduliwa kwa kitabu cha mwongozo wa namna bora ya ufugaji wa nyuki hapa nchini kwa lengo la kuwapatia fursa wafugaji wa nyuki kufanya kazi hiyo kwa miongozo inayotolewa na serikali ili kupata mazao bora ya nyuki.

Waziri  Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda  akiwa na viongozi mbambali wakiwa wameshika  kitabu cha mwongozo bora   wa ufugaji nyuki kilichozinduliwa wakati wa maadhimisho ya siku ya nyuki Duniani yaliyofanyika  Kitaifa Mkoani  Katavi kwenye uwanja wa michezo wa Azimio Mjini Mpanda.

Mwakalukwa amesema serikali kwa pamoja wanaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafugaji Nyuki hapa nchini ili sekta hiyo iwe chanzo kikubwa cha Mapato katika Taifa la Tanzania.

Madhimisho ya Siku ya nyuki Duniani yamefanyika mkoa wa katavi Kitaifa na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa mazao ya Nyuki ambapo wadau wazao la nyuki walipata fursa ya kueleza umuhimu wa mazao ya nyuki katika ukuaji wa uchumi kwa Taifa.

   

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages