Na Walter MguIuchuma, Katavi
Mkoa wa Katavi umefanikiwa kusajili watoto 50,197 waliochini ya Umri wa miaka mitano katika mpango wa kuwasajili kupitia Utekelezaji Mpango wa kusajili vizazi kwa watoto wenye Umri chini ya miaka Mitano.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usajili,Ufilisi na Udhamini (RITA)Makao Makuu Angela Anatory wakati wa kikao cha tathimini ya zoezi hilo la usajili kwa Mkoa wa Katavi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Maji.
Mkoa wa Katavi ulianza Uandikishaji huo Novemba mwaka jana na hadi sasa usajiri umefikia asilimia 34 katika Mkoa.
Amebainisha kuwa kabla ya zoezi hilo kufanyika katika Mkoa wa Katavi ulikuwa na asilimia 6.3 ya watoto waliosajiliwa hivyo hatua hiyo nimafakio kwa Mkoa wa katavi na RITA kwa ujumla kwani kutasidia watoto hao kutopata changamoto za viambata na nyaraka kama hizo wakiwa wakubwa katika shughuli mbalimbali.
Katika hatua nyingine Angela amesema Mpango wa usajili wa watoto ni moja ya mikakati iliyobuniwa kuhakikisha wanafikiwa wananchi wengi zaidi ili waweze kusajiliwa na taarifa zao kuhifadhiwa kwaajili ya matumizi mbalimbali ambapo Mpango huu unatekelezwa katika Mikoa 22 ya Tanzania Bara ambapo zaidi ya watoto Milioni 7.5 wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa hapa nchini.
Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa katavi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akihutubia katika kikao cha Tathimini hiyo amesema Usajili na utambuzi wa watoto kupitia Mpango huo wa RITA utapunguza changamoto za usumbufu kwa watoto wanapokuwa katika hatua mbalimbali za ajira na mambo ya kiserikali kwakuwa watakuwa na vitambulisho tambuzi kama cheti cha kuzaliwa na hivyo wazazi na jamii kwa ujumla lazima kushiriki vyema katika zoezi hilo.
Buswelu ameeleza kuwa Mpango huwa kupitia RITA pamoja na serikali katika Mkoa wa Katavi umeanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka jana huku huduma hiyo ikiwa inatolewa bure kwa wananchi na wazazi wenye watoto chini ya Umri wa miaka Mitano katika Mkoa wa Katavi.
Alifafanua kuwa Mkoa kabla ya zoezi hili awali ulikuwa katika asilimia 6 na sasa kufikia asilimia 34 bado safari ipo ya kufikia asiimia100 na kupitia kikao hicho Mkoa upo tayari kuzipokea changamoto zilizojitokeza kwenye zoezi hilo ili kuona namna bora ya utatuzi na malengo ya serikali ya zoezi hilo yatimie kama inavyo kusudiwa.
Buswelu aliongeza kuwa Mkoa wa Katavi umekuwa na mwingiliano na wageni kutoka nchi za jirani hivyo zaoezi hilo nivyema likafanyika katika mazingira ya Umakini mkubwa ili kuepuka kutoa vitambulisho vya kuzaliwa kwa watoto wasio sitahili kupatiwa vitambulisho hivyo.
Kwa upande wao Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri za Mkoa wa Katavi wameeeleza kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo katika zoezi hilo ni baadhi ya wazazi au walezi kutokuwa na vitambulisho vya Urai au namba za nida hali inayopelekea baadhi ya watoto kushidwa kupatiwa vitambulisho hivyo.
Wameshauri kuwa ili kufikia mafanikio ya zoezi hilo nivyema mamlaka zinazo husika kuharakisha mpango wa kuwapatia namba za Nida ili watoto wao wapate usajili wa RITA na vitambulisho vya kuzaliwa.
Mkoa wa katavi ni miongoni mwa Mikoa inayotekeleza zoezi la kusajili watoto waliochini ya umri wa miaka Mitano zoezi hilo lilianza Mwaka jana Mwezi Novemba kwa Usimamizi wa Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini(RITA).
![]() |
| Wajumbe wakiwa katika kikao cha Tathimini ya zoezi la usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano lililofanyika Mkoani Katavi kuanzia Mwezi Novemba mwaka jana |

