MWENYEKITI MTEPA CCM TUTAENDELEA KUSHIKA DOLA KWA KUWATII WATU

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Method Mtepa akizungumza na wajumbe wa chama hicha mara baada ya kuchaguliwa.-(Picha na Paul Mathias).

Na George Mwigulu,Mpanda.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Method  Mtepa amesema heshima ya  CCM kushika dola ni lazima kuendelea kukubalika kwa kuwatii,kuwaheshimu  na kuwatendea watu yale wanayodhani yanawafaa.

Baadhi ya wajumbe wa CCM  wilaya ya Mpanda wakiwa kwenye zoezi la kuchagua viongozi ngazi ya wilaya.- (Picha na Paul Mathias)

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Method  Mtepa amesema heshima ya  CCM kushika dola ni lazima kuendelea kukubalika kwa kuwatii,kuwaheshimu  na kuwatendea watu yale wanayodhani yanawafaa.

Kauli hiyo ameitoa  baada ya kukamilika kwa uchanguzi wa ndani ya chama hicho ngazi ya wilaya katika uwanja wa CCM-Azimio,Manispaa ya Mpanda mkoani hapo,  mara baada ya kutangazwa mshidi alieleza kwenye uongozi wake atahakikisha masirahi ya watu yanapatikana.

Mtepa alifafanua kuwa chini ya uongozi wake utakwenda kwa kasi kubwa na yuko tayari kufanya kazi na mtu yeyote anayependa maendeleo na mwenye nia  ya kweli ya kuheshimu wenzake  na masirahi yao.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa katika zoezi la upigaji Kura katika uchaguzi uliofanyika Uwanja wa CCM Azimio-(Picha na Paul Mathias) 

“...hili ndio tatizo langu kama wewe ni kiongozi hujali masirahi ya kiongozi mwenzako na wewe ni kiongozi hutaki kujali maagizo na maazimio  ya Chama Cha Mapinduzi kwa mwanachama wako,kwakweli utaniona ni mwiba” amesema  Mwenyekiti huyo.

Vilevile amewaomba  Wananchama wasijitenge kwa kudhania kuwa kazi imekwisha bali kwa sasa kazi ndiyo imeanza, Sababu waliowatangulia kwenye uongozi wake wako makini kutizama mwenedo wao wa kufanya kazi ya maendeleo ya watu hivyo hatakubali kujipaka matope.

Aidha amewasisitiza  wananchama na wepenzi wa CCM kutambua kuwa yeye sio Malaika wala si Mungu bali anategemea ushauri wao  kwani binafsi hana mbinu za kufikiri na kujiamulia mwenyewe binafsi.

Awali katika uchaguzi huo,Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa ngazi ya wilaya ya Mpanda,Aniset Lwamba akitangaza matokeo ya uchaguzi kwa nafasi  ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya,Amemtangaza Method Mtepa kuwa mshidi kwa kupata kura 532 huku wapizani wake Emmanuel Manamba akipata kura 150 na Mweji Jinyam akipata kura 150.

Msimamizi Mkuu wa uchaguzi CCM Wilaya ya Mpanda,Aniset Lwamba akitangaza Matokeo ya uchaguzi wa viongozi Mbambali ngazi ya wilaya ambapo amemtangaza ,Method Mtepa kuwa mwenyekiti Mpya wa CCM Wilaya ya Mpanda-(Picha na Paul Mathias)

Idrasa Sultani,mmoja wa wajumbe wa chama hicho baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi amesema kuwa CCM ni chama kinachozingatia demokrasia na kuwa mfano kwa vyama vingine huku akiwaomba kuiga mfano huo kwa vitendo.

Sultani alieleza kuwa kwa sasa wanakazi moja pekee ya kuwatumikia wananchi ili kuwaletea maendeleo kwani kazi ya chama inafanywa vizuri ya kuisimamia serikali.

Anna Onesmo aliwaomba wananchama wa CCM kuondoa tofauti zao zilizotokana na makundi ya kiuchanguzi bali waendelee kuwa na mshikamano.

Amesisitiza kuwa ummoja na mshikamano ni siri ya mafanikio kwa watu wenye nia moja ya kuendelea kushika dola na kuwatumikia wananchi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages