Baadhi ya wataalamu ambao wako wanafanya tathimni wa kiufundi namna ambavyo daraja hilo litakavyojengwa. |
Na Walter Mguluchuma,Tanganyika .
WAKAZI wa Mishamo Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi wataondokana na changamoto ya muda mrefu ya kusafiri umbali mrefu kwa kutumia baiskeli au kutembea kwa miguu kwenda kununua samaki na mafuta ya mawese katika mwambao wa Ziwa Tanganyika baada ya ujezi wa daraja la kuuganisha mkoa wa Kigoma kuanza kujengwa.
Kujengwa kwa daraja na barabara hiyo kutakuwa ni mkombozi wa wananchi wa Mikoa ya Katavi na Kigoma katika kuinua uchumi wa wananchi hao na taifa kwa ujumla .
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) Mkoa wa Katavi,Mwandisi Martini Mwakabende amesema kuwa daraja hilo kubwa la aina yake litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni mbili.
Amebainisha kuwa katika katika ujenzi wa madaraja yaliyojengwa na kusimiwa na TANROADS Mkoa wa Katavi hilo ni daraja la pili kwa ukubwa na lililotumia gharama ya fedha nyingi daraja la kwanza ni la mto Koga linaloiunganisha Mikoa ya Katavi na Tabora .
Amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kukamilika mwezi wa pili mwakani 2023 na mradi huu unatekelezwa na Kampuni ya ujenzi ya MSELEM CIVIC ENG CONST y a Mkoani Rukwa.
Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo kutoka kwenye Kampuni hiyo Uwesu Salum Uwesu ameeleza kuwa licha ya kipindi cha masika kuwa karibu uanze wanatarajia kumaliza mradi huo kwa wakati .
Mkazi wa Mlibasi Evaristi Noribo alisema kuwa kukamika kwa daraja hilo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Mishamo walikuwa wakilazimika kutembea kwa miguu kwa muda wa siku mbili hadi kufika mwambao mwa Ziwa Tanganyika kwa ajiri ya kufatia samaki ,dagaa na mafuta ya mawese.
Amesema kuwa yeye ameishi kwenye eneo la Kijiji hicho toka mwaka 1975 hivyo anaona ni kama ndoto kujengwa kwa daraja hilo muhimu kwa uchumi wa wananchi wa mikoa ya Katavi na Kigoma