MUWASA YAKABIDHI PIKIPIKI 30 KWA WAFANYAKAZI WAKE KUIMARISHA UTENDAJI KAZI

 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza na watumishi mbalimbali wa idara ya maji Manisipaa ya Mpanda wakati akikabidhi pikipiki kwao zenye jumla ya thamani ya Mil 99

Na Paul Mathias,Mpanda.

Mamlaka ya Maji  safi na usafi wa Mazingira Muwasa Katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi imepatiwa pikipiki 30 na Serikali Zenye Samani ya shilingi Milion 99.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizindua zoezi la ugawaji wa pikipiki 30  kwa wataalamu mbalimbali wa idara ya maji Manispaa ya Mpanda.

Mamlaka ya Maji  safi na usafi wa Mazingira Muwasa Katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi imepatiwa pikipiki 30 na Serikali Zenye Samani ya shilingi Milion 99.

Akikabidhi pikipiki hizo kwa niaba ya Serikali katika hafla iliyofanyika Ofisi za Muwasa Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi Mkuu wa Mkoa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema pikipiki hizo zikatumike kwa lengo lililokusudiwa ili kuendelea kutoa huduma kwa wanachi nasio kwenda kufanyia Shughuli Binafsi.

Mwanamvua amesema katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma mbalimbali kwa muda unaotakiwa Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais samia Suluhu Hassan imekuwa ikiendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyakazi kwa kuwapatia vyombo vya Usafiri kama pikipiki na vifaa vingine kwa Madhumuni ya kuimalisha ufanisi wa kazi kwa Wafanyakazi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akikabidhi funguo za pikipiki kwa mlengwa Christina Mbula.

Katika hatua nyingine Mwanamvua amesema amekuwa anapokea malalamiko kutoka kwa wananchi ya kubambikiziwa Bili za maji kwa wateja kutoka mamlaka ya Muwasa na kuwaomba kutumia pikipiki hizo zilizotolewa na serikali kuwafikia wateja wao kwa Kusoma Mita zao kwa wakati ili kupunguza malalamiko hayo kwa wateja wao.

Katika hafla hiyo amesisitiza Utaratibu wa Mgao wa Maji kusimamiwa kwa utaratibu unaoeleweka na kusiwepo na aina yeyote ya kwenda kinyume na Utaratibu wa Mgao huo wa Maji hali amabayo huwaathili watumiaji wa huduma hiyo kwa kukosa Huduma hiyo kwa wakati.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa Rai kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya Maji kwani uwepo wa vyanzo hivyo ndio unafanya huduma ya maji kupatikana kwa wananchi na Kuziomba mamlaka zinazohusika na masuala ya uhifadhi kuendelea kusimamia kikamilifu sharia zinazo husu Usimamiaji wa Uhifadhi wa mazingira na Misitu katika mkoa wa katavi.

Awali akisoma Taarifa ya Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira [MUWASA] Mkurugenzi wa mamlaka hiyo  Manispaa ya Mpanda Eng Hussein Nyemba  amesema anaishukuru wizara ya Maji kwa kuwapatia pikipiki hizo amabazo zitasaidia kulinda Vyanzo vya Maji,pamoja na kuhudumia wateja kwa haraka na kusaidia kuziba Mivujo ya Maji na kuizibiti kwa haraka.

Mkurugenzi wa MUWASA,Eng Hussein Nyemba akitoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanmvua Mrindoko.

Nyemba amebainisha kuwa kuwa vyombo hivyo vya usafiri vitasaidia katika ukusanyaji wa Mapato kwa Taasisi hiyo na kuisadia katika makusanyo ya Maduhuri ya serikali kwa haraka tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha sharia za usalama barabarani hazikiukwi kwa Maafisa waliopewa Pikipiki hizo walipewa elimu juu ya sheria za usalama barabarani kwa kushirikiana na ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ili watumishi hao watumie vyombo hivyo kwa usitadi unaotakiwa kwa kuzinagatia sharia za usalama barabarani.

Nao baadhi ya watumishi waliopatiwa pikipiki hizo akiwemo Bwana Lema  Jeremia Meneja ufundi Muwasa amesema wanamshuru Rais Samia suluhu hassan kwa kutatua changamoto ya usafiri ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa muda Mlefu hali iliyopelekea kuwa na changamoto kubwa ya utendaji kazi za kila siku.

Jeremia amebainiha kuwa walikuwa wanachelewa kuwahudumia wateja wao kwa kuchelewa kufika kwenye Mivujo ya maji na kuiziba kwa wakati huku ujio wa pikipiki hizo utakuwa mkombozi kwao na watafanya kazi kwa bidii.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages