Paul Mathias na George Mwigulu,Nsimbo.
Viongozi wa chama cha Mapinduzi ccm mkoa wa Katavi wameaswa kudumisha umoja na mshikamano ili chama hicho kiendelee Kushinda katika chaguzi na kuwa tumikia wananchi kwa weledi kwa vitendo.
![]() |
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi,Idd Kimanta akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe kwenye kikao mkutano mkuu maalumu. |
Viongozi wa chama cha Mapinduzi ccm mkoa wa Katavi wameaswa kudumisha umoja na mshikamano ili chama hicho kiendelee Kushinda katika chaguzi na kuwa tumikia wananchi kwa weledi kwa vitendo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Idd Hassan Kimanta wakati akiwa hutubia
wanachama wa Chama hicho katika Mkutano Mkuu maaalumu wa Utekelezaji wa Ilani
ya Chama cha Mapinduzi CCM Katika Jimbo la Nsimbo Wilaya ya Mpanda katika
ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondary Nsimbo.
Katika
hotuba yake Kimanta alisema Umoja na mshikamano katika chama hicho katika mkoa
wa Katavi ndiyo silaha pekee ya kukifanya chama hicho kuendelea kuaminiwa na wananchi
kwa kuwaletea Maendeleo.
![]() |
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye maadamano ya mkutano maalumu. |
![]() |
Wanachama wa CCM wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Nsimbo Mkoa wa Katavi wakati wa mkutano mkuu maalumu wa jimbo la Nsimbo. |
![]() |
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi,Futunata Kabeje (Kulia) akiwa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Katavi,Matha Maliki wakiwa kwenye mkutano mkuu maalumu wa Jimbo la Nsimbo. |
![]() |
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Katavi,Abdrahaman Kilo (wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu maalumu wa Jimbo la Nsimbo. |
Mwenyekiti huyo amewashukia vikali baadhi ya viongozi Madiwani ambao wamekuwa na Tabia za kutoheshimu Mamlaka za viongozi wengine ikiwemo viongozi wa Vijiji kwa Kuwabeza huku baadhi yao wakitoa amri za kuondoka kwenye nafasi zao hali ambayo inaenda kinyume na Utaratibu na miongozo ya uongozi.
Ameeleza
kuwa uongozi wake utakuwa uongozi shirikishi kwa kila kundi la watu kwakuwa
msingi mkubwa wa kufanikiwa katika uongozi ni ushirikiano kwa kuwa chama cha
Mapinduzi kinaamini katika kuwatumikia wanachi kwa vitendo.
Alisisitiza
kuwa Jukumu la Diwani katika kata yake nikuhakikisha anasimamia vyema miradi ya
maendeleo kwa kuwa shirikisha wanachi kwakuwa wao ndio wanufaika wakubwa wa
Miradi hiyo.
![]() |
Baadhi ya viongozi wa Mkuu wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye mkutano mkuu maalumu wa Jimbo la Nsimbo. |
Alibainisha
kuwa kunabaadhi ya viongozi hususani Madiwani kuwa na Tabia ya kuzizalau kamati
za maendeleo ya kata na kusema huo sioungozi na chama hakita sita kuwachukulia
hatua za kinidhamu watakao bainika kufanya vitendo hivyo.
Katika hatua nyingine kimanta amesema viongozi
wa chama katika mkoa wa Katavi waliochaguliwa katika uchaguzi ulifanyika mwaka
huu wajiandae kupatiwa mafunzo maalumu ya uongozi ili zikianza hatua
kuchukuliwa kusiwe na Kisingizio cha viongozi kutojua baadhi ya mambo yanayohusu
chama hicho kiutendaji.
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe katika hotuba yake amesema kwa kipindi cha Miaka miwili iliyopita kumekuwa na mafanikioa makubwa katika sekta za afya,Elimu,Miundombinu,Elimu, na Maji kwa Msukumo wa Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Fedha za maendeleo kwa kasi kiasi cha Shilingi Bilion 10 na Milioni 823 katika Jimbo la Nsimbo.
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe akiwahutubia wananchama na wapenzi wa chama hicho kwenuye mkutano maalumu wa Jimbo la Nsimbo. |
Katika kuhakikisha kazi za chama cha Mapinduzi CCM katika Jimbo la Nsimbo zinaendelea kuimalika Mbumge huyo alisema atanunua Pikipiki 12 kwa Mkatibu wa Kata wa chama hicho huku Makatibu Tawi akiahidi kuwanunulia Baiskeli na Kuahidi kutoa kiasi cha shilingi Milioni kila Kata ili kusaidia kazi za chama kwenye kata hizo.
Katika
Sekta ya michezo kwa Kipindi cha Miaka miwili Lupembe alibainisha kuwa ametumia
kiasi cha shilingi milioni 109.6 kwaajili ya ununuzi wa Jezi,Mipira,na zawadi
kwa washindi katika mashindano ya Lupembe Cup na Lupembe Sensa Cup 2022.
Mkutano mkuu huo maalumu ulikuwa na lengo la kusoma Taarifa za utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM katika Jimbo la Nsimbo zilizofanywa na serikali kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo na watendaji wa Halmashauri hiyo kwa ujumla.