MADARASA ELFU KUMI NA MBILI KUJENGWA NCHINI


Wahadhili wa Chuo Kikuu cha Dodoma  akiwawezesha washiriki  wa mradi wa Boost.

Na Kibada Ernest -GCO Mlele

Jumla ya vyumba vya Madarasa 12,000 vya Shule za Awali na Msingi hapa nchini vinatarajiwa kujengwa kwa kipindi cha miaka mitano kupitia Mradi wa BOOST katika maeneo yenye upungufu au Msongamano wa Wanafunzi.

Jumla ya vyumba vya Madarasa 12,000 vya Shule za Awali na Msingi hapa nchini vinatarajiwa kujengwa kwa kipindi cha miaka mitano kupitia Mradi wa BOOST katika maeneo yenye upungufu au Msongamano wa Wanafunzi.

Akifungua Mafunzo elekezi ya utekelezaji wa Mradi huo wa kuwajengea wajumbe wa timu za utekelezaji wa Mikoa na Halmadhauri kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu ambayo ni Mbeya,Katavi,Songwe na Rukwa waliokutana Mbeya Shule ya Wasichana Sekondar Loleza,Mratibu wa Mafunzo kutoka OR-TAMISEMI Yusuph Singo Omari ametaja thamani ya Mradi huo kuwa ni Trilioni1.15 Kwa nchi nzima.

Mratibu huyo ameleza kuwa utekelezaji wa Mradi huo utakuwa wa lipa kwa matokeo,hivyo timu za utekelezaji zitapaswa kufanya kazi kwa matokeo ili kuwezesha Mradi kuendelea na kusaidia kuondoa changamoto zilizopo katika Elimu ya Awali na Msingi.

Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wake,Mradi wa BOOST unatarajia kujenga vyumba vya madarasa 12,000,kutoa vifaa vya TEHAMA kwa Shule za Msingi na Vituo vya Mafunzo kwa Walimu 8000,mpango wa Shule salama 6000,kuongeza uandikishaji wa Elimu ya Awali kufikia asilimia 85 ya uandikishaji ifikapo 2026.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Loleza yakiwakutanisha Wataalam wapatao 281 wa halmashauri ktk Mikoa minne wa sekta ya Elimu,Mipango,Uhandisi,Mawasiliano Serikalini,Manunuzi,M/Jamiii na nyinginezo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages