WATUMISHI MLELE WATAKIWA KUHAMIA KWENYE MAKAZI MAPYA.

 


Waziri Mkuu akisalimiana na mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mapili mara baada ya kumaliza kuwatubia wananchi baada ya kumaliza kukagua barabara

Na Kibada Ernest –Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali Mlele.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Mlele wahamie mara moja kwenye nyumba 11 zilizokuwa za wajenzi wa barabara ya Inyonga-Mpanda hadi Tabora na kukabidhiwa kwa Halmashauri hiyo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Mlele wahamie mara moja kwenye nyumba 11 zilizokuwa za wajenzi wa barabara ya Inyonga-Mpanda hadi Tabora na kukabidhiwa kwa Halmashauri hiyo.

Watumishi ambao ameagiza wahamie kwenye nyumba hizo ni Afisa Usalama wa Wilaya (DSO), Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mlele {OCD}, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele (DED), Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini {TARURA} Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mlele {DMO} pamoja na watumishi wengine wa hospitali ya wilaya.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo   wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi baada ya kujionea mwenyewe kuwa zimetelekezwa na zinaharibika kwa kukosa uangalizi.

“Watumishi wanahangaika hawana makazi, nyumba zimeachwa nyasi zimeota hadi kwenye korido. Watumishi wote wanaopaswa kuhamia katika nyumba hizi baada ya kumaliza mkutano huu kila mmoja aende kwenye  Nyumba yake na ahamie. Mkurugenzi naomba orodha ya majina ya watakaohamia.”

Nyumba hizo 11 zenye ukubwa tofauti kati yake mbili zina uwezo wa kuchukua familia nne kila moja ni za kisasa na zilikabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlele Novemba 2022 na Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS baada ya kukamilika kwa Mradi wa barabara.


Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameutaka uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele uweke utaratibu wa kushirikisha wadau wa sekta binafsi katika kuleta maendeleo kwenye wilaya yao. Pia aliwataka watumishi hao wahakikishe kila kazi wanazozifanya zinakuwa na matokeo chanya kwa jamii.

 Awali, Waziri Mkuu alikagua barabara ya lami ya kutoka Inyonga-Mapili yenye urefu wa kilomita 11.7 iliyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 8.69. Barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Inyonga-Ilunde-Kishelo inayokwenda hadi kwenye mpaka wa Mkoa wa Katavi na Tabora ikiwa na urefu wa kilomita 96.

Wakizungumza baada ya ukaguzi huo, baadhi ya wakazi wa eneo la Mapili walimshukuru Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo kukamilika kwake kutaimarisha huduma za usafiri wa watu na mizigo.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages