Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia wakazi wa Halmashauri ya Mlele katika Kijiji cha Mapili mara baada ya kukagua barabara |
Na Walter Mguluchuma,Mlele.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua barabara ya kiwango cha lami ya Inyonga Mapili yenya yenye urefu wa zaidi ya kilometa 11 iliyogharimu shilingi bilioni 8.69 itayosaidia kuondoa changamoto kwa wajawazito walikuwa nayo ya kuchewa kufika Hospitali pindi walipokuwa wameshindwa kujifungua na kupelekea baadhi yao kupoteza uhai.
Mwandisi Izack Kamwele mara baada ya kuelezea manufaa ya barabara ya lami ya Inyonga Mapili mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua barabara ya kiwango cha lami ya Inyonga Mapili yenya yenye urefu wa zaidi ya kilometa 11 iliyogharimu shilingi bilioni 8.69 itayosaidia kuondoa changamoto kwa wajawazito walikuwa nayo ya kuchewa kufika Hospitali pindi walipokuwa wameshindwa kujifungua na kupelekea baadhi yao kupoteza uhai
Babarabara hiyo ni sehemu ya barabara Inyonga,Ilunde Kishelo hadi Kitundaambako kuna mapanda njia ya barabara za kwenda Mbeya na Singida pamoja naTabora . .
Akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mlele mara baada ya kakagua Babara hiyo Waziri Mkuu Kassim alisema kuwa ameridhishwa na kiwango cha ubora wa ujenzi wa barabara hiyo .
Amebainisha kuwa lengo la ujenzi wa barabara hiyo ni kuiunganisha hadi kwenye makutano ya barabara za Mikoa ya Tabora na Singida.
Na itawafanya wananchi wa Halmashauri ya Mlele kusafiri kwa kupitia njia hiyo kwenda Mkoani pasipo kulazika kupitia Mpanda ambapo ni mbali zaidi .
Muonakano wa barabara aliyokagua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ya Inyonga Mapili |
Amewakata wananchi waitunze vizuri barabara hiyo kwani ni mkombozi kwa wananchi
Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mapili Domick Mbaruku amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutowa fedha za ujenzi wa barabara hiyo .
Kwani kukamika kwa barabara hiyo kutakuza uchumi wa wananchi na kwa Taifa na kutaimarisha huduma za usafiri wa watu na mizigo.
Anna John anaishukuru Serikali kwa kuwajali husunani wananchi wa hali ya chini wakati wa masika mvua zikinyesha magari yalikuwa hayafiki na vifo vya wajawazito vilikuwa vingi kwani walikuwa hawafiki hospitali kwa wakati .
Walikuwa wakipata wagonjwa usiku walikuwa wanalazimika kuwabeba kwa machela wagonjwa wao .
Mbunge wa Jimbo la Katavi Mwandisi Izack Kamwele alisema barabara hiyo ni muhimu sana kwa wananchi wa Mikoa ya Katavi,Tabora na Singida na kwa Watanzania.