DALA DALA WALALAMIKIA BAJAJI KUINGILIA NJIA ZAO.



Baadhi ya Daladala zinazofanya kazi ya kusafirisha abiria kutoka kituo cha zamani cha Mabasi Mpanda Mjini hadi vikonge wakiwa eneo lao la kazi kwaajili ya kusafirisha abiria[Picha na Paul Mathias]
Na Paul Mathias 

Waendesha Daladala wa Magari Madogo (haice) katika Barabara ya Mpanda Kigoma wamelalamikia mamlaka ya usafirishaji wa Majini na  nchikavu Mkoa wa Katavi Latra kwa kushindwa kuzizuia  Bajaji kufanya kazi kutoka Mpnda mjini hadi Vikonge wilaya ya Tangayika hali ambayo imewafanya kukosa wateja kutokana na mwingiliano huo.

Madreva wa Gari ndogo zinazofanya safari zake kutoka Mpanda Mjini hadi Mpanda ndogo wakiwa kituo cha zamani cha Mabasi Mpanda mjini wakisubiria Abiria[Picha na Paul Mathias]
Waendesha Daladala wa Magari Madogo (haice) katika Barabara ya Mpanda Kigoma wamelalamikia mamlaka ya usafirishaji wa Majini na  nchikavu Mkoa wa Katavi Latra kwa kushindwa kuzizuia  Bajaji kufanya kazi kutoka Mpnda mjini hadi Vikonge wilaya ya Tangayika hali ambayo imewafanya kukosa wateja kutokana na mwingiliano huo.

Wamebainisha hayo kwa nyakati tofauti kuhusu tatizo hilo wamesema kuwa wamekuwa   wakishangazwa na hali hiyo kwa Bajaji kufanya kazi kwenye njia hiyo hadi eneo la Vikonge kwa kuwa lipo Wilaya ya Tanganyika na siyo ndani ya Manispaa ya Mpanda na kuasabisha kukosa abiria.

James Thadeo Dereva wa Daladala Mpanda mjini hadi Majalila wilaya ya Tanganyika anasema kuwa tatizo linalowatatiza wao ni Bajaji kupatiwa kibali cha kufanya kazi na Latra kwenye barabara hiyo hadi Mpanda ndogo umbali wa Zaidi ya kilometa 25 wakati huo na wao wakiwa kwenye njia hiyo na kuasabisha kudolola kwa biasahara yao kutokana na uwepo wa Bajaji hizo.

‘’sisi kero yetu ni Bajaji kwenda Mpanda ndogo tumepewa Latra kutoka hapa kwenda Mpanda ndogo hadi vikonge latra tena wanatoa Kibali kwa Bajaji kwenda Mpanda ndogo hadi vikonge je nisheria ipi inayo ruhusu bajaji kwenda hadi huko kutoka hapa mjini tulitaka sisi tujue kutoka hapa hadi vikonge ni Kilomita 38 kikawaida bajaji ilitakiwa zifanyekazi ndani ya Manispaa ya Mpanda’’amesema James

Kwa upande wake Salivius Sebastiani Dereva anaefanya kazi ya usafirishaji kwa Daladala kutoka Mpanda ndogo Kwenda Mpanda Mjini amesema tatizo kubwa njia yao ya vikonge kuingiliwa na Bajaji na wao kushidwa kufanya kazi yao kwa uhakika kutokana na ukosefu wa wateja.

‘’njia ya Mpanda ndogo vikonge imeingiliwa na Bajaji kwa hiyo changamoto ya Biashara imekuwa ngumu kazi hakuna Bajaji zimetuzidi nguvu kwa hiyo tulitaka kupata majibu juu ya Bajajipamoja na Daladala leseni zetu kama zinaingiliana huenda tuwaache wafanye biashara maana sisi imeshindikana hakuna wateja’’

 Fransinsiko Kadogo Dereva wa Daladala kutoka Mpanda Mjini hadi Majalila anasema ‘’kero yetu kubwa ni suala la Bajaji kuwa na Latra Mbili ambapo anakuwa anatoka hapa mpka vikonge hadi Majalila ukiangalia hadi sasahivi Gari zetu za Mpanda dogo zimepungua kutoka Gari 22 hadi kubakia Gari 10 siku moja masaa 24 zinatoka gari Mbili nasisi tunafamilia watu saidie’’ amesisitiza Kadogo.

Amebainisha kuwa msimu wa mapato umekaribia kwa hali ilivyo sasa kuna uwezekano mkubwa wa wamiliki wa Haice wakashindwa kulipa mapato kutokana na kukosa wateja wa abiria ambao wengi wao sasa wanapanda bajaji

Allen Mwaniri Meneja Mfawidhi wa Latra Mkoa wa Katavi amesema kuwa kwa mujibu wa sheria hakuna chombo cha usafirishaji kinacho ruhusiwa kuwa na Njia mbili kwa wakati mmoja.

Gari ndogo zinazofanya kazi ya kusafirisha Abiria Kutoka Mpanda Mjini Hadi Vikonge[Picha na Paul Mathias]

“kwanza cha kwanza chombo chotekile kinachotoa huduma hakiwezi kutoa Leseni zaidi ya Moja kama ameomba Leseni Manispaa ya Mpanda hatakiwi kwenda kwa hiyo sheria ni kwamba awe na Leseni Moja tu kuomba Leseni nyingine  kwenye halmashauri nyingine’’

Mwaniri ameeleza kuwa mwezi uliopita kulikuwa na kikao baina ya Maafisa usafirishaji na Mkuu wa mkoa na miongoni mwa malalamiko yaliyojitokeza ni suala hilo la Bajaji kwenda Mpanda ndogo na kuazimia kuwa Bajaji hizo ziendeleaa kufanya kazi kama makubaliano ya kikao cha mwaka juzi kilivyo ridhia cha Bajaji kutoka Nje ya Manispaa ya Mpanda.

Meneja huyo wa Latra amesma mwezi uliopita kulikuwa na kikao na Mkuu wa Mkoa na hao wadau wa usafishaji wa Bajaji na Daladala malalamiko yalikuwa ndiyo hayo lakini maazimio ya kawa ni amabayo yalishawahi kutolewa mwaka juzi kwa ngazi ya DC na kile kikao cha mkuu wa mkoa kubariki  maazimio yaendeleevilevile.

‘’Bajaji ambazo zinaleseni ndani ya Manispaa zitafanya kazi Barabara ya Nsimbo,Zita enda Itenka,zitakwenda Barabara ya Kigoma Majalila kule ila zisiingie kama zinaenda Mwese na wala zisiende Kasekese ndicho tulichokubalina hicho’’ amesema allen.

kwa habari zaidi tembelea Ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com       

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages