Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stuart Kiondo akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa umma mbele ya Waandishi wa Habari [PICHA na Paul Mathias] |
Na
Walter Mguluchuma,Katavi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imebaini kuwepo kwenye miradi iliyotekelezwa katika Halmashauri mbambali za Mkoa huu ikiwa na upungufu wa Zaidi ya Shilingi Bilioni 2.1 na wameweza kuchukua hatua mbambali kwenye miradi hiyo .
Waandishi wa Habari mkoa wa Katavi wakiwa katika majukumu yao wakati taarifa ya utendaji kazi ya Takukuru ikitolewa ofisini hapo[Picha na Paul Mathias] |
Amebainisha kuwa Takukuru Mkoa wa Katavi katika kipindi hicho
cha miezi mitatu ya October na Decembe
Mwaka 2022 wameweza kufatilia miradi
yenye thamani ya shilingi
Bilioni 5 katika sekta
za ujenzi,elimuna afya .
Katika ufatiliaji huu wa miradi
kwenye Mkoa huu wameweza kubaini miradi
yenye thamani Sh,2,170,000,000 ikiwa na
mapungufu kwenye miradi iliyotekelezwa katika Halmashauri mbambali za Mkoa huu.
Kiondo amesema
kati ya shilingi Bilioni 5 zilizotolewa kati hiyo shilingi Bilioni 1. 12 zilitolewa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt Samia
Suluhu Hassan zijulukanazo Pochi la Mama .
Waandishi wa habari mkoa wa Katavi wakisikiliza Taarifa ya utendaji kazi wa Takukuru ofisini hapo[Picha na Paul Mathias] |
Naibu Mkuu huyo wa Takukuru
ameitaja baadhi ya miradi hiyo ni miradi
yenye upungufu ni mradi wa ujenzi
wa jingo
la ICU na nyumba za watumishi
Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika
yenye thamani y ash,340,000,000 miradi hiyo ilikutwa na mapungufu
yakuweka matofali yasiyo na kiwango na ukiukwaji wa taratibu
za manunuzi na tayari uchunguzi
umeanza .
Uujenzi wa kituo cha Afya
Itenka Halmashauri ya Nsimbo wenye
thamani ya wenye thamani y ash
,530,000.000,ujenzi wajengo la dharura
Hospitali ya Halmashauri ya Nsimbo
sh 300,000,000 na ujenzi wa
majengo matano Bohari , mionzi jingo la utawala , jingo la mama na
mtoto na jingo la kufulia nguo yenye
thamani y ash 1,000,000,000 Hospitali ya Nsimbo .
Amesema kasoro walizozibaini ni ukiukwaji wa
taratibu za manunuzi na ucheleweshaji ambapo uchunguzi wake tayari
umeanza na waliweza kubaini matofali matofali yalitumika kwenye ujenzi
hayakuwa na ubora baadhi ya kuthibishwa .
Kiondo ameeleza kuwa katika kipindi cha robo ya kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu wanataraji kuongeza juhudi za kuimarisha kuzuia rushwa kwa kufatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhamasisha kutoa elimu kwa wananchi ya ushiriki wa kupiga vita rushwa .
Na wataendelea
kufatilia kwa karibu fedha
zote zinazotolewa na Serikali
ili kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa na upande
wa miradi kuwa bora na thamani ya fedha kuonekana .
Kiondo amewataka wananchi wa Mkoa wa Katavi
kutoa taarifa mara moja pindi ambapo wanapokuwa wanapigiwa simu na watu
ambao ni matapeli wanao kuwa
wamewapigia simu na kujifanya wao ni Maafisa wa Takukuru kwa lengo la
kuwatishia na kutaka kujipatia pesa.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
https://kataviclub.blogspot.com/