SERIKALI ZA MITAA VINARA MALALAMIKO YA RUSHWA KATAVI


Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stuart Kiondo akitoa taarifa ya utendaji kazi ya Takukuru Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha October -December 2022[PICHA na  [George Mwigulu.]

Na Paul mathias- Katavi

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru  Mkoa wa katavi Kwa kipindi Cha mwezi October Hadi December 2022  imepokea Malala Miko 65 kutoka Taassi mbalimbali za Umma.

Waandishi wa habari Mkoa wa katavi wakitekeleza majukumu yao wakati Naibu mkuu wa Takukuru mkoa wa Katavi Stuart Kiondo akitoa taarifa mbele yao[Picha na George Mwigulu]

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru  Mkoa wa katavi Kwa kipindi Cha mwezi October Hadi December 2022  imepokea Malala Miko 65 kutoka Taassi mbalimbali za Umma.

Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa katavi Stuart Kiondo amesema kuwa Kati ya Malalamiko hayo 65 malalamiko 58 yalihusu Rushwa na 7 haya kuhusu Rushwa.

Kiondo amebainisha kuwa Taasisi za Serikali za mitaa imeongoza Kwa kuwa na malalamiko 30 Huku Idara ya Aridhi ikiwa na malalamiko 4, na Polisi mamalamiko 2.

Katika taarifa hiyo Taasisi za Afya  zimelipotiwa kuwa na malalamiko 4, huku ushirika ikiwa na malalamiko miko 2 na malalamiko binafsi 3.

Taassi za  Mahakama,Tanesco,NSSF,Tarula,Maji,TRA,na Mazingira zikiwa na lalamiko Moja Kila Mmoja.

Taarifa hizo zimeanza kushughulikiwa Kwa kuanzisha uchunguzi Kwa mujibu wa Sheria ya ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 sura ya 329.

Katika hatua nyingine Kiondo amesema majalada 3 ya uchunguzi wa wazi yamefunguliwa na majalada 10 ya uchunguzi yamekamilika.

Waandishi wa Habari mkoa wa Katavi wakisikiliza utaoaji wa Taarifa ya Takukuru kwenye ofisi za Takukuru Mkoa wa Katavi[Picha na George Mwigulu]

Amesema Mashauri 3 yamefunguliwa Mahakamani huku shauri 1 limetokana na taarifa zilizopokelewa Kwa kipindi cha October -December 2022 na kufanya jumla ya kesi 8 zinazoendelea Mahakamani na hakuwa na kesi yoyote iliyo iliyotolewa maamuzi Hadi Sasa.

Takukuru katika kuendelea kufanya Kazi kazi Karibu na wanachi imekuja na Mfumo Mpya unaojulikana kama TAKUKURU _Rafiki yenye lengo la kuongeza ushiriki wa Kila mwananchi na wadau katika kikabiliana na tatizo la Rushwa katika utoaji wa Huduma Kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mfumo huu unatajwa kuwa na faida Kwa kuchangia kukuza usitawi wa utawala Bora Kwa kuzuia vitendo vya Rushwa visitokee katika utoaji wa Huduma Kwa umma au katika utekelezaji wa Miradi ya maendeleo.

Hii itachangia kuboresha huduma zinazotolewa Kwa umma na wadau wengine kuokoa fedha za umma Kwa kujengwa au kutekelezwa miradi Bora inayokidhi thamani ya fedha iliyotumika.

kwa habari zaidi Tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages