![]() |
Wanachama wa umoja wa watuma salamu Wilaya ya Mlele wakiwa katika kituo cha afya Inyonga kwaajili ya kuwafariji wagojwa. |
Mwenyekiti
wa umoja wa watuma salamu wilaya ya mlele Maganga peter amesema kuwa wao kama
watuma salamu wamewiwa kufanya matendo ya huruma kwa kuwaona wagojwa hao
hospitalini hapo
‘’mimi
nimeona nivyema sana kama mwenyekiti wa salamu klabu wilya ya Mlele kwa sababu
huu ni mwezi wa kwarezima lakini pia tunaenda mwezi wa ramadhani,unapotoa kitu
unajiwekea akiba kwa mwenyezi Mungu kwa sababu ni mwezi wa toba wagojwa
wamefarijika kwa kile tulichojaliwa kuwapatia’’amesema Maganga
Pius
kipeta Mwenyekiti wa Katavi salamu club amesema kuwa jamii ijenge umuhimu wa
kuwatembelea wagojwa na kuwafaliji kwakuwa Maradhi kwa mwanadamu nisehemu ya
maisha hivyo kila mmoja anaowajibu wa kuwafariji wagojwa kwa kadri
alivyojaliwa.
Mganga
mfawwidhhi wa kituo cha afya Inyonga Gilishi Jonh amewashukuru watuma salamu hao kufika hospitalini
hapo kwa kuja kuwafariji wagojwa.
Wanachama wa umoja wa watuma salamu wamesema wataendelea kuwa karibu na jamii ili kuonyesha upendo kwakuwa wao ni sehemu ya jamii ya wanatania.