![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akiwasili katika ofisi za Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza wakuu wa idara za Serikali katika Mkoa wa Ktavi kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa wandishi wa Habari wanapokuwa katika Majukumu yao
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko aliekaa katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waaandishi wa habari mkoa wa katavi alipotembelea ofisini hapo |
Agizo hilo amelitoa wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali vya Habari vilivyoko katika Mkoa wa Katavi kwenye ofisi ya Klabu ya Wandishi wa Habari Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake aliyoifanya.
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Katavi mwanamvua Mrindoko akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari Mkoa wa Katavi baada ya kutembelea ofisi za klabu ya waandishi wa habari mkoa wa katavi |
Mrindoko ameeleza kuwa wandishi wa habari wa Mkoa wa Katavi wanafanya kazi kubwa ya kuutangazo Mkoa wa Katavi ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa na wamekuwa
wakifanya kazi kwa uzalendo mkubwa kwa
kujitoa bila kujali muda wala umbali wa eneo wanalokwenda kufanyia kazi.
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akabidhiwa taarifa ya klabu ya waandishi wa Habari iliyosomwa na Paschal Katona katibu wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Katavi. |
Kwa kutambua mchango wa wanndishi yeye kama mkuu wa Mkoa anawahidi kuwapatia pikipiki mbili ambazo ambazo zitawasaidia kuzitumia kwenda kwenye maeneo na kuweza kufika kwa haraka kwenye matukio hasa kwenye maeneo ya pembeni mwa mji kwani kwa sasa wanalazimika kuwa wanatumia usafiri wa kukodi hali ambayo imekuwa ikiwafanya washindwe kufika kwa wakati .
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akisalimiana na waandishi wa Habari mkoa wa Katavi alipotembelea ofisi ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Katavi. |
Mwenyekiti wa Chama hicho Walter Mguluchuma amesema waandishi wa Habari wapo tayari kuendelea kufanya kazi za kushirikiana na Serikali kwa lengo la kuhabarisha umma na kusaidia kuweza kuleta maendeleo ya kweli katika mkoa wa Katavi.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameahidi kutoa Pikipiki Mbili kwaajili ya klabu ya waandishi wa Habari pamoja na kutoa kiasi cha shilingi Milioni Mbili kwaajili ya kusaidia klabu ya waandishi wa habari katika mkoa wa Katavi.