![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akiongoza kikao cha kamati ya amani na maridhino Wilaya ya Mpanda chenye lengo la kudumisha amani. |
Akizungumzakwenye kikao hicho
kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu huyo wa wilaya Jamila
amesema kuwa wakati wa kampeni na wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 29
Oktoba 2025 Wilaya ya Mpanda haikuathirika na Vurugu ya aina yeyote.
“Ndugu viongozi tutakumbuka kuwa Wilaya yetu
ya mpanda haikupata taharuki wala aina yoyote ya vurugu kabla ya kampeni,wakati
wa kampeni wakati wa Uchaguzi na hata baada ya Uchaguzi tofauti na baadhi ya maeneo
mengine hapa nchini’’DC Jamila
“nitumie nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru
viongozi wote viongozi wa Dini,viongozi wa vyama vya siasa walioko hapa,waandishi
wa Habari na Wananchi wote wa Mpanda kwa Umoja wao kwa sala na dua lakini umoja
na mshikamano nao umesababisha kuleta Amani katika Wilaya yetu ya Mpanda”
Amesema Jamila.
Aidha DC Jamila ametoa Rai kwa
Viongozi wote wa Dini ,Vyama vya Siasa pamoja na Waandishi wa Habari
kuhakikisha kuwa wanaendelea kuhubiri umuhimu wa Amani ndani ya wilaya ya
Mpanda na Taifa zima kwa ujumla huku akitolea mfano jinsi Baba wa taifa hayati
Mwl.Nyerere alivyojenga Taifa la Tanzania kwa misingi ya Amani na Mshikamano.
“Nikushukuru sana Mhe.mkuu wa
wilaya kwa kazi nzuri uliyoifanya pamoja na wajumbe wote wa kikao hiki kwa kazi
nzuri ambayo mmeifanya kabla wakati na baada ya uchaguzi,kazi ile mliyoifanya
ndiyo imetufanya hapa leo tutembee kifua mbele huku tukiutaja mkoa wetu kwamba
uchaguzi umekwenda salama na mkoa umebaki salama,hii yote ni matunda ya kazi
nzuri ambayo tumeifanya” Amesema Mchungaji wa Kanisa la Moravian Mpanda Mjini.
Kamati ya amani na maridhino Wilaya ya Mpanda inaudwa na Viongozi wa Dini,vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa vyama vya siasa.



