Na Walter Mguchuma,Mpanda.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wanaofanya kazi ya kupakia taka ngumu kwenye Maeneo mbambambali ya Halmashauri ya Manispaa Mkoa wa Katavi wapo hatarini kupatwa na magonjwa mbambali ya kuambukiza kutokana na kufanya kazi hiyo pasipo kuwa na vifaa vya kujikinga kama vile Maski.
![]() |
Kama unavyoona kwenye picha hao ni wafanyakazi wa kuokota taka ngumu wakiendelea na kazi yao,Lakini hawana mavazi yoyote ya kujinda na afya zao. |
Wafanyakazi wanaofanya kazi ya kupakia taka ngumu kwenye Maeneo mbambambali ya Halmashauri ya Manispaa Mkoa wa Katavi wapo hatarini kupatwa na magonjwa mbambali ya kuambukiza kutokana na kufanya kazi hiyo pasipo kuwa na vifaa vya kujikinga kama vile Maski.
Wakiongea na mwandishi wa Habari wakati wakiwa wanaendelea kufanya shughuli hiyo leo hii kwenye Maeneo ya Manispaa hiyo wamedai kuwa kilio cha wao kukosa vifaa kimekuwa cha muda mrefu sasa na swala hilo wamesha lifikisha kwa uongozi wa Manispaa hiyo lakini hakuna jitihada ambazo zimefanyika hadi sasa .
Mmoja wa wafanyakazi hao jina tunalo aliyekuwa akipakia taka nguvu kwenye Roli la Manispaa hiyo lenye Namba za usajiri SM 12244 ameeleza kuwa wapo hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza kutokana na shughuli wanayofanya ya kupakia taka wakiwa hawana vifaa wanavyopaswa kuwa navyo vya kujikinga ili wasiweze kupata maladhi mbambali .
Amebainisha kuwa licha ya wao kuomba wapatiwe vifaa vya kujikingia kwa muda mrefu sasa Manispaa imekuwa haiwajali hali ambayo inawafanya kwa kiasi kikubwa kuwa hatarini kupats magonjwa.
"...kazi hii ni ngumu sana inahitaji umakini mkubwa wakati unaifanya,suala la kujilinda dhidi ya afya zetu linategemea sana vifaa maalumu vya kutetendea kazi hasa kuvaa...nashangaa kwa nini uongozi wa manispaa hawalitambui hilo nauliza ni nini kusudi lao?.Je ni kuona tunapata magonjwa?" amehoji kwa uchungu mmoja ya wafanyakazi hao.
Amefafanua kuwa baadhi yao wenyeuwezo wameanza kujinunulia viatu aina ya gun but ingawa kwenye kundi lao walioweza kununua viata hivyo hawazidi watatu .
Amesesema wanashangazwa na Halmashauri ya Manispaa kuweza kushindwa kuwapatia hata maski ambazo gharama zake ni ndogo mmno hivyo wanaomba waangalie uwezekano wa kupatiwa vifaa husika vya kufanyia kazi ili waepukane na hali ya sasa ya kuwa hatarini kupatwa na magonjwa yakiwepo ya mlipuko .