Katavi .
Taasisi ya PASS TRUST ambayo
inayoshughulika na kuwawezesha wajasirimali wote ambao
wapo kwenye mnyororo wa kilimo wamezindua kampeni ya
Kijanisha Maisha katika Mkoa wa Katavi ili kuunga juhudi za
Serikali na Dunia kwa ujumla katika swala zima la kutunza
mazingira hasa kwenye sekta ya kilimo ambacho ni sehemu kubwa ya
nchi nchi na inayotowa ajira na kipato
katika Nchi yetu ya Tanzania .
Baadhi ya washiriki wa kongamano la wadau wa sekta ya kilimo katika Mkoa wa Katavi walipokuwa kwenye kongamano la kilimo lililoandaliwa na PASS TRUST liliofanyika katika ukumbi wa Lyamba Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.
Taasisi ya PASS TRUST ambayo inayoshughulika na kuwawezesha wajasirimali wote ambao wapo kwenye mnyororo wa kilimo wamezindua kampeni ya Kijanisha Maisha katika Mkoa wa Katavi ili kuunga juhudi za Serikali na Dunia kwa ujumla katika swala zima la kutunza mazingira hasa kwenye sekta ya kilimo ambacho ni sehemu kubwa ya nchi nchi na inayotowa ajira na kipato katika Nchi yetu ya Tanzania .
Uizinduzi huu katika Mkoa wa Katavi umezinduliwa
katika mkutano maalumu ambao uliwashilikisha wadau wa sekta ya kilimo
uliofanyika katika ukumbi wa Lyamba katika Manispaa ya Mpanda na
uliwashilikisha wadau wa kilimo kutoka katika Halmashauri zote tano za Mkoa wa
Katavi
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Pass
Trust Hermani Bashiri ambae ni meneja wa maendeleo ya biashara
amesema kuwa uzinduzi uliofanyika Mkoani Katavi ni mwendelezo tuu wakampeni
ambayo imeisha zinduliwa tayari hivyo aliwahakikishia
wanafika kwenye kila Mkoa na kwenye kila Wilaya hapa Nchini ili
wadau wao wote waweze kupata taarifa na kuweza kuchukua furusa hii ya kijani
shirikishi .
Amefafanua kuwa Pass Trust ni asisi ya kusaidia
sekta binafsi ya kilimo ni chombo ambacho kilianzishwa mwaka
2000 ili kuchochea uwekezaji na kukuza kilimo cha
biashara na sekta zinazo husika katika mnyororo wa kilimo
.
Amebainisha kuwa walengwa wakubwa kwenye mradi huu
ni wajasiriamali wote ambao wapo kwenye mnyororo wa kilimo
kuanzia mtu binafsi mmoja mmoja au kwa njia ya vikundi vilivyosajiriwa na
Halmashauri na taasisi nyingine ambazo zinashughulika na kilimo na
mnyororo wake wa thamani ya kilimo .
Bashiri ameeleza kuwa wanawajibika katika utoaji
wa huduma za maendeleo ya kilimo cha biashara kwa
,wajasiriamali wadogo na wakati kwa kuwaunganisha na taasisi
za fedha ambao mpaka sasa wanafanya kazi na taasisi za kifedha Zaidi ya kumi
nan nne hapa nchini .
Amesema kuwa pia malengo yao PASS
Trust ni kuchochea uwekezaji na kuhimiza ukuaji wa
kilimo nchini Tanzania na dira yao ni kuwa
asasi inayoongoza katika utoaji wa huduma za
fedha na maendeleo ya biashara katika sekta ya kilimo hapa
nchini .
Kuhusu huduma za fedha watawasaidia
watu na makampuni wanaositahili kupata mkopo kwa
ajiri ya uwekezaji wenye faida kupitia tathimini ya
maandiko ya kuwaombea mikopo kulingana na benki husika .
Amesema kipaumbele kitatolewa kwawatejawenye
matokeo makubwa katika mwendelezo wa mnyororo
wa thamani wa bidhaa za kilimo husani katika mazao ya
chakula ,biashara na mazao ya kusafirishwa nje .
Nae Neema Zakaria mmoja wa wadau wa sekta ya kilimo
ameshukuru kwa taasisi hiyo kwa kuweza kufika
Mkoani Katavi na kufanya kongamano ambalo limeambatana na
mafunzo ambayo yamekuwa tija kubwa sana kwao kwa ajiri ya kufanya
biashara zao za mnyororo wa kilimo ..
Edward Mlanda amewashukuru PASS kwa furusa
waliowaletea ambayo hawakuwa nayo wao hasa wakulima wengi walikuwa wanashindwa
kuchukua mikopo kulingana na mazingira lakini sasa kwa
udhamini wa PASS Sasa watanufaika .
Amewaomba wakulima wenzake wa Mkoa wa Katavi wasiogope
kuchukua mikopo kwa kutokuwa na mdhamana kwani
sasa mdhamini PASS wameisha jitokeza bila
kujari wametokea kwenye mazingira gani huo kwao ni msaada mkubwa
sana kwa wakulima
Afisa kilimo wa Mkoa wa Katavi Faridu Abdalla
amesema kuwa kuna changamoto mbali mbali amzazo zimekuwa zikiwakabili vijana wa
Mkoa wa Katavi kwenye sekta ya kilimo miongoni mwa changamoto hiyo
ni vijana wengi kutokuwa na umiliki wa ardhi .
Pia vijana wengi wamekuwa na mtazamo hasi kwenye
kilimo kwa kudhani kuwa shughuli ya kilimo hufanywa na wazee tuu jambo
ambalo sio la kweli .
Changamoto nyingine ameeitaja kuwa ni vijana
kutotambua furusa za uhuhimu wa kilimo na pia wamekuwa
wakishindwa kuumudu gharama za uwendeshaji wa shughuli za kilimo kutokana
nakuwa na uwezo mdogo wa kiuchumi .
Amesema kuwa Mkoa wa Katavi bado hauja tumia furusa
inavyotakiwa kwenye sekta ya kilimo kwani kuna ekari laki tisa ambazo
zinafaa kutumika kwa shughuli za kilimo lakini kati ya ekari hizo ni ekari laki
mbili na nusu tuu ndio zinazotumika kwa shughuli za kilimo kwenye Mkoa
huu.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Neemia James
Katibu Tawala msaidizi Uchumi na Uzalishaji
wa Mkoa wa Katavi amewataka wananchi wa Mkoa wa Katavi kutumia
furusa ya uwepo wa PASS katika kuboresha shughuli zao za kilimo na usindikaji
wa mazao yao mbambali watakayo kuwa wanazalisha .
Kubwa Zaidi ni swala la mikopo taasisi hiyo inawasaidia wakulima na wasindikaji wa mazao mbali mbali kwenye kuboresha kilimo chao na shughuli za usindikaji hali ambayo itawafanya waongeze pato lao na kufanya shughuli zao za kilimo kwa uhakika mkubwa .