MANISPAA YA MPANDA LAWAMANI KUSHINDWA KUNUNUA VIFAA VYA WAZOA TAKA

.
Baadhi ya wafanyakazi wa kubeba taka wakiwa majukumu yao ya kazi leo kwenye maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
 
Na George Mwigulu,Mpanda.

Wafanyakazi wa kubeba taka katika mitaa ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wako hatari kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosa vifaa maalumu vya kujikinga na uchafu huo wakati wakipakia kwenye gari.


Wafanyakazi wa kubeba taka katika mitaa ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wako hatari kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosa vifaa maalumu vya kujikinga na uchafu huo wakati wakipakia kwenye gari.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao,Baadhi ya wafanyakazi hao wakiwa kwenye gari la kubeba taka namba SM 12244 wamedai kuwa na mazingira magumu zaidi ya kufanya kazi hiyo na kusababisha hofu ya kutokuwa salama kiafya.

“…pamoja na kufanya kazi kwenye mazingira haya,Manispaa imeona jambo la kawaida kutuacha kuendelea kufanya kazi kwenye hali hii mbaya ambapo hatuelewi ni lini tena tutapewa vifaa vingine” amesema mmoja ya wafanyakazi wa kubeba taka.

Wamebainisha kuwa miezi michache iliyopita waliweza kununuliwa vifaa vipya kwa ajili ya kujikinga kama vile Viatu vigumu,Maski na Gloves za mikononi,Lakini pekee ni viatu vigumu vilivyodumu hadi sasa wanavitumia ikiwa vingine vimehalibika kutokana na kutokuwa na ubora unaotakiwa.

Mfanyakazi mmoja amesema kuwa kufanya kazi bila vifaa hivyo sio ni hatari kwao pekee bali inawaondolea pia nguvu na thamani yao kama binadamu kufanya kazi kwenye mazingira hayo “…binafsi najisikia vibaya sana,Mkurugenzi chukua hatua kunusuru afya zetu”.

Mmoja wa Mkazi wa Manispaa ya Mpanda,Wande Mashala amesema viongozi wa Manispaa ya Mpanda wanapaswa kuhakikisha wanalinda afya za wafanyakazi hao kutokana na kuwa nao ni wategemewa na familia zao kwani wakipata magonjwa watashindwa kuwajibika kwa familia zao.

Amesema kuwa ni aibu kwa manispaa kuwa na wafanyakazi ambao suala la afya zao ziko hatarini kupata magonjwa ya mlipuko ili hali suala hilo liko ndani ya uwezo wao.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages