Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Nassoro Kakulukulu akizungumnza na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Katavi wakati wa Sikuu kuu ya Eid El Adha |
Balaza la waislamu Tanzania Bakwata Mkoa wa Katavi limesema kuwa linaunga mkono juhudi mbalimbali za kimaendeleo zinazo fanywa na serikali kupitia uwekezaji na ubinafsishaji wenye lengo kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Balaza la waislamu Tanzania Bakwata Mkoa wa Katavi limesema kuwa linaunga mkono juhudi mbalimbali za kimaendeleo zinazo fanywa na serikali kupitia uwekezaji na ubinafsishaji wenye lengo kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na shekhe mkuu wa mkoa wa Katavi Mashaka Nassoro Kakulukulu wakati akiongoza swala ya Eiad El Adha iliyoswaliwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Kashato MpandaKakulukulu
amsema ‘’Kuna mambo mbalimbali ambayo serikali inatuletea katika mikakati yake
na mipango yake nilazima na niwajibu wetu kuiamini na kutii yale ambayo
yanayoletwa letwa kwetu ‘’
‘’yapo
mambo mbalimbali ambayo serikali inayafanya katika nchiyetu yapo mambo
mbalimbali ambayo yanaelekezo la serikali katika nchi yetu kwa mujibu wa aya
hii twatakiwa sisi kuwa tii na na kuelekea katika maelekezo ambayo wanayatoa’’amesema
Kakulukulu
Katibu tawala mkoa wa Katavi Abas Hassan Rugwa akitoa salamu za serikali katika sikukuu ya Eid El Adha viwanja vya shule ya Msingi Kashato |
‘’Serikali
haiwezi kutuletea jambo ambalo linamadhara kwetu mfano katika mambo ya
uwekezaji serikali haiwezi kuleta jambo ambalo jambo hilo inafahamu kwamba
litaleta madhara kwa wananchi wake ikiwa serikali italeta jambo lenye madhara
hiyo serikali itawaongoza akinanani‘’
Katika
taua nyingine amewaasa waumini wa Dini ya kiislamu na wananchi wa ujumla kuishi
katika utii,Umoja na mshikamano pamoja
‘’Ibaada
yetu hija inatufundisha kuwa na umoja kuwa na mshikamano kuwa na umoja wa Umma
watazame waloko hija leo hauwezi ukamtambua mfalme hauwezi ukamtambua waziri
hauwezi ukamtambua rais wote wapo kwenye vazi moja hakika umati huu ni umma
mmoja’’
‘’niwaombe
sana tuendelee kuzingatia mila na tamaduni na maadili yetu yote ya kiimani nay
ale mengine ya kijamii ili kuifanya jamii yetu iwe salama zaidi’’
Baadhi ya waumini walioshiriki swala hiyo wamesema kuwa niwajibu wa jamii kuendelea kusisitiza malezi bora kwa watoto na kuwalea katika misingi ya kumcha mungu ili kuwa na kizazi chenye hofu ya mungu.