MBUNGE MARTHA KUTOA MIL 29 KUKWAMUA UWT KATAVI.

 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Maliki akizungumza na wanawake wa UWT Wilaya ya Tanganyika wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo ameahidi kutoa fedha cha fedha Mil 29 kwa Jumuiya hiyo.

Na Paul Mathias,Katavi.

Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Katavi wameahidiwa kupewa kiasi cha fedha Milion 29, Na Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa huo Martha Maliki ambapo fedha hizo zitasaidia jumuiya kujikwamua kwenye mdodoro wa kiuchumi.

Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Katavi wameahidiwa kupewa kiasi cha fedha Milion 29, Na Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa huo Martha Maliki ambapo fedha hizo zitasaidia jumuiya kujikwamua kwenye mdodoro wa kiuchumi.

Martha Maliki amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kikazi akiwa anazungumza na wananchi leo katika Kata ya Karema,Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi akiwa na lengo la kukagua uhai wa UWT.

Mbunge huyo wa Viti maalumu ameweka wazi kuwa licha ya kuahidi kutoa kiasi cha fedha Mil 29 ambazo zitalenga kata zote 48 za Mkoa wa Katavi,ameamua hapo hapo kutoa fedha Tsh 500,000/- kwa UWT Karema ili kuonesha namna gani amedhamilia kuwasaidia wanawake ili kufikia adhima yao ya kukua kiuchumi.

“…mwanamke ni nguzo kubwa kwenye jamii,kumwezesha ni suala muhimu kwa msitakabali wa maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla” Ameeleza Martha kuwa huo ndio msingi wa kutoa fedha hizo.

Martha amesisitiza “Kama mfumko wa Jumuiya itaimarika zaidi itakuwa rahisi wanawake kujikopesha fedha za kutosha ambazo zitabeba uhalisi na maana kamili ya fedha ambayo mwanajumuiya itamwezesha kufanya mambo makubwa zaidi ya kimaendeleo”.

Katika hatua nyingine ya kuimarisha Jumuiya hiyo ametoa kadi 200 za chama hicho kwa jumuiya ya UWT Kata ya Karema ambazo zitawasaidia kuendelea kusajili wanachama wapya ambao watakaifanya jumuiya hiyo kuwa kubwa zaidi.

Asha Haruna, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Tanganyika licha ya kumshukuru Mbunge wa Viti Maalumu huyo amesema msaada huyo wa Tsh 500,000/- utakuwa chachu kwa wanawake hao kuizalisha fedha hizo kibiashara ili wanawake wengine waweze kunufaika kupitia mikopo.

“…Niwaase wanawake wenzangu,fedha hizi mkazisimamie kikamilifu kupitia biashara ndogondogo ili mpate kunufaika kwa kuinua maisha yenu” Amesema Asha.

Katika ziara hiyo Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi, Martha Maliki ametembelea Kata ya Kapala,Msenga na Karema kwa kuongea na wananchi pamoja na kuwaeleza mipango ya serikali ya kuwaletea maendeleo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages