MBUNGE MARTHA AOMBA WANANCHI WASIUZE ARDHI KIHOLELA TANGANYIKA


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Maliki (wa tano kutoka kulia) akiwa katika bandari ya Karema,Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi  wakati wa ziara yake ya kikazi- (Picha Na Paul Mathias)

Na George Mwigulu,Katavi.

Wakazi wa Kata ya Karema,Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi  wameombwa kutouza ardhi yao  kiholela  kwa bei ya chini kwani ujio  wa bandari ya Karema utapandisha thamani ya ardhi hali itakayo saidia kuinuia maisha yao siku za usoni.

Wakazi wa Kata ya Karema,Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi  wameombwa kutouza ardhi yao  kiholela  kwani ujio  wa bandari ya Karema utapandisha thamani ya ardhi hali itakayo saidia kuinuia maisha yao siku za usoni.

Ombi hilo limetolewa leo na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki wakati wa ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Tanganyika ambapo ameeleza wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari ya kulinda ardhi yao wenyewe kwa kutokuwa na tamaa ya pesa.

Martha amefafanua kuwa thamani ya ardhi hupanda bei kila siku hivyo kwa watu wanaopenda mafanikio ya kiuchumi kipaombele chao huwa ni kulida ardhi huku ardhi hiyo wakitumia kwenye fursa ya uzalishaji mali kama vile kilimo na ujenzi wa nyumba za makazi na biashara.

“…niwaombe wananchi wa Karema tusiuze ardhi yetu kiholela,Ardhi hii itakuwa ya thamani sana hapo baadaye kwenu kutokana na badari hii…tusiuze ardhi ndugu zangu” Amesema Martha.

Mbunge huyo wa viti maalumu ameeleza kuwa uimarishwaji wa miundombinu ya barabara ya Kabungu Karema inayoelekea bandari ya Karema tayari serikali imeshatoa tangazo la tenda ya ujenzi ambapo barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami.

Ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhakikisha shughuri za maendeleo zinarahisishwa hususani usafirishwaji wa bidhaa,maligafi, mazao ya chakula na biashara kuelekea nchini  Congo ambapo bandari ya Karema ni kiungo muhimu.

Mbunge huyo amesisitiza “… niishukuru serikali ya Dkt Samia Suluhu  Hassain kwa kuamua kujenga barabra hii ya Kabungu Karema kwa kiwango cha lami kwani kutachochea ukuaji wa kiuchumi wa Mkoa wa Katavi”.

Kwa upande wake Afisa wa Bandari ya Karema,Mhadisi  Angetile Mwasasu amesema kuwa banadari hiyo imekamilika Kwa asilimia 90 na tayari huduma mbalimbali zimeanza kutolewa.

“kwa sasa wako maafisa mbalimbali mahali hapa kama vile Idara ya uhamiaji,TRA na maafisa wengine ambao wanatekeleza majukumu yao ya kuhakikisha kazi zinaenda bila matatizo,Hivyo natoa wito kwa wafanya biashara wa Mkoa wa Katavi kufanya uwekezaji ili wapate kunufaika kupitia bandari” Amesema Mhadisi huyo.

Diwani wa Kata ya Karema,Maiko Kapata amemuomba rais Samia Suluhu Hassan kuwaletea meli itakayowasaidia wananchi kufanya shughuri za kiuchumi kwenye hali salama.

Amesema wananchi wengi kwa sasa baadhi yao hutumia usafiri wa boti katika shughuli zao hali ambayo wakati mwingine husabisha vifo na hasara kibiashara kwa kuzama na boti hizo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages