Na Paul Mathias,Mpanda
Wananchi katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameobwa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru unaotalajia kuanza Kukimbizwa Wilaya ya Mpanda Mnamo 25 /8/2023.
Wananchi katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameobwa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru unaotalajia kuanza Kukimbizwa Wilaya ya Mpanda Mnamo 25 /8/2023.
Akitoa taarifa ya maandalizi ya
kuelekea kuupokea Mwenge huo katika kikao kazi kilicho fanyika Ukumbi wa
Mikutano wa Manispaa ya Mpanda Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema
Mwenge wa Uhuru unatalajia kukimbizwa katika Halmashauri zote mbili za Wilaya
ya Mpanda, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmshauri ya Nsimbo.
Mwenge huo wa Uhuru unatalajia
kukibizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda 25/8/203 na 26/8/2023 Katika
halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda.
Amesema katika Manispaa ya
Mpanda Miradi yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 1 na Milioni 774 huku
Halmashauri ya Nsimbo miradi itakayofikiwa na Mwennge wa Uhuru itakuwa na
Thamani ya Shilingi Milioni 897 na 52 Elfu .
Katika hatua nyingine Mkuu huyo
wa Wilaya amesema Mwenge wa uhuru utazindua miradi mbalilmbali ya Maenndeleo
katika Wilaya ya Mpanda.
‘’tunavyo vyumba viwili vya
Madarasa kule halmashauri ya Nsimbo vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 40 upo
mradi wa Maji Kapanda wenye thamani ya Shilingi Milioni 265 laki mbili na
arobaini na Saba,Zahanati ya Matandalani kule stalike yenye thamani ya
Shilingi Milioni 60,Vyumba vitano vya
Madarasa shule ya Msingi Misunkumilo yenye thamani ya Shilingi Milioni 130 ‘’amesema
Jamila yusuph Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa
miradi mbalimbali itawekewa Mawe ya Msingi na Mwenge huo wa Uhuru miradi hiyo
nipamoja na Ujenzi wa Barabara ya Lami Mita 745 halmashauri ya Nsimbo yenye
thamani ya shilingi milioni 494 na elfu sabini na Tisa na mianane,Shule ya
Mchepuo wa kiingereza yenye Thamani ya Shilingi Milioni 160 ,Kituo cha Afya
Kazima Jengo la OPD,Maabara na Jengo la kichoma taka vyenye thamani ya Shilingi
Milioni 250.
Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka
2023 Ubeba Kaulimbiu isemayo Tunza
Mazingira okoa vyanzo vya Maji kwa usitawi wa Viumbe hai na Taifa kwa Ujumla.