Na George Mwigulu,
Tanganyika.
WATU 8,400 wa kijiji cha Vikonge na Kitongoji cha Inyagantambo kilichopo katika kijiji cha Majalila Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameondokana na changamoto ya maji safi na salama baada ya mradi wa maji Vikonge kuanza kuwahudumia.
Mradi
huo ambao ulianza kutekelezwa katika kijiji cha Vikonge May, 2022 na kukamilika
na kuanza kutoa huduma Nov, 2022 umezinduliwa na kiongozi wa mbio za mwege wa
uhuru kitaifa,Abdalla Shaib Kaim ambapo gharama za ujenzi wa mradi huo ni fedha Tshs 608,603,837/= zimetumika.
Meneja
wa RUWASA wilaya ya Tanganyika Mhadisi, Alikam Sabuni akitoa leo taarifa ya
ujenzi wa mradi wa maji Vikonge mbele ya kiongozi wa mbio za mwege wa uhuru kitaifa
Abdalla Shaib Kaim amesema kuwa manufaa ya mradi huo utahakikisha upatikanaji
wa huduma ya maji safi na salama katika zahanati ya kijiji cha Vikonge na
kuondoa maradhi yatokanayo na matumizi ya maji yasiiyokuwa safi.
Alikam ameeleza kuwa mradi huo unaimarisha mahudhurio ya wanafunzi mashuleni hasa katika shule ya msingi Vikonge pamoja na unarahisisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika soko la kijiji cha Vikonge.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Mlele,Majid Mwanga(kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Michael Ngayalina (kulia). |
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,Jamila Yusuph (Kushoto) akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru baada ya kuongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Katavi katika mapokezi ya Mwenge huo. |
“Tunamshukuru
rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha zinazowezesha ujenzi wa mradiiiii
huu ambao umetatua kero ya maji kwa matumizi ya nyumbani na shughuli nyingine
za kiuchumi” Amesema Meneja huyo.
Kiongozi
wa Mbio za Mwege wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim akizindua mradi wa maji
Vikonge amesema kuwa licha ya mradi huo umelenga kumtua mwanamke ndoo kichwani lakini
suala la kulinda vyanzo vya maji linapaswa kuzingatiwa.
Abdalla
amesema kulinda vyanzo vya maji ni pamoja na kudhibiti shughuli za wanadamu zinazoendelea
kwa kuzingatia kanuni,taratibu na miongozo inayoelekeza kwenye vyanzo vya maji
lazima umbali wa mita 60 uzingatiwe.
Kiongozi
huyo wa mbio za mwege wa uhuru kitaifa amewataka viongozi wa wilaya ya
Tanganyika kusimamia kwa kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi ya serikali ya
vijiji ambapo ametoa muda wa wiki mbili kufika tamati na kupata suluhisho
litakalo ondoa shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.
Aidha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi umezindua miradi saba yenye thamani ya Tshs 1,502,734,107/=.
Baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Katavi waliohudhuria katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru leo katika viwanja vya shule ya msingi Vikonge halmashauri ya wilaya ya Tanganyika. |
Baadhi ya Viongozi na watumishi mbalimbali wa Mkoa wa Katavi wakiwa wanasubili kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru leo katika viwanja vya shule ya msingi Vikonge ambapo mwenge huo ukitokea Mkoa wa Kigoma. |
Awali
akipokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Vikonge wilaya ya Tanganyika Mkoani
hapa,Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ambaye ni Mkuu wa
Wilaya ya Mlele Majid Mwanga amesema kuwa katika Mkoa wa Katavi mwenge wa Uhuru
utaenda kupitia miradi jumla ya 40.
Mwanga
amesema kuwa miradi 22 utaweka mawe ya msingi katika miradi 8 na utakabidhi
misaada,kutembelea miradi 10 na thamani ya miradi hiyo ni fedha zaidi ya Bil
8.818 ikiwa halmashauri ya Tanganyika ni miradi 7 ya fedha zaidi ya Bil 1.502,Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda miradi 11 yenye thamani ya fedha zaidi ya Bil 1.77.
Vile
vile katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo miradi 10 yenye gharama ya fedha
zaaaidi ya Mil 897.052, halmashauri ya wilaya ya Mlele miradi 8 yenye gharama
ya fedha zaidi ya Mil 653.15 pamoja na halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe miradi
4 yenye gharama ya fedha zaidi ya Bil 3.991.