Mwanzilishi na Mkurugenzi NeoLife International.Veronica Biaka akizungumza na wajasiriamali wa Mkoa wa Katavi katika ukumbi wa New Katavi Resort Manispaa ya Mpanda. |
Na George
Mwigulu, Katavi.
MWANZILISHI na Mkurugenzi wa Taasisi ya NeoLife International kanda ya Magharibi,Veronica Biaka amesema dhana ya usawa wa kijisia sio kukandamiza jinsi yeyote bali ni kuweka mfumo mzuri utakaosaidia kuwa na fursa sawa kwa jinsi zote.
Veronica Biaka,Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya NeoLife International akizungumza na wajasiliamali. |
Dhana ya usawa wa kijinsia
ndani ya jamii ya Mkoa wa Katavi imekuwa ikitafasiriwa kuwa na lengo la
kumgandamiza mwanaume ambaye amekuwa kiongozi kuanzia ngazi ya familia.
Veronica ametoa kauli hiyo
leo katika ukumbi wa New Katavi resort Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakati
akizungumza kwenye kongamano la wajasiriamali ambapo amewaondoa hofu wanaume na
kuwataka kuwapa fursa wanawake ya kujikwamua kiuchumi.
Mkurugenzi huyo wa Neolife International amesema
baadhi ya watu wengi hawafahamu dhana ya usawa wa kijisia,wengine wanahusisha
usawa wa kijinsia na ubaguzi au kulinda
kundi moja katika jamii jambo ambalo sio kweli na linarudisha nyuma jitihada za
usawa ndani ya jamii.
Amefafanua kuwa wanaume wanapaswa kuepuka kufanya vitendo vya ukatili wa kiuchumi dhidi ya wanawake bali wanapaswa kuwa viongozi wa kweli ndani ya familia kwa kutoa usawa wa umilki mali mbalimbali.
Aidha amewaondoa hofu wanaume kwamba katika zama hizi mwanamke akipewa fursa ataweza kusaidia familia yake.
" Kuna changamoto nyingi za kiuchumi ndani ya familia,kama wakutegemewa atakuwa mwanaume pekee iko siku anaweza kuugua magonjwa kama vile kupooza na nk,Je kama yeye ndiye mwenye jukumu la kuzalisha uchumi wa familia akipatwa na maradhi hayo nani ataisaidia" Ameuliza Mkurugenzi huyo.
Vilevile amewaomba wanawake wasidanganyike pindi wanapokuwa na uwezo wa kifedha na kukimbilia kuishi pake yao kwani maisha hayo ni magumu sana hivyo wanapaswa kuishi kwa kuheshimiana ndani ya ndoa na mafanikio wanayoyapata yawe kwa ajili ya familia.
Ameeleza kuwa NeoLife International imedhamilia kuuweka ulimwengu mzima kuwa wenye afya tele na wenye furaha.Hivyo kutokana na changamoto za lishe ndani ya jamii wanahamasisha tiba kupitia vyakula ambavyo vinaondoa matatizo ya afya.
Rebeca Paul,Moja ya mfanyabiashata mwanamke ambaye amefanikiwa kujikwamua kiuchumi baada ya kuamua kusubutu na kuwezeshwa na NeoLife International. |
Meneja wa Bank ya Azania
Tawi la Tunduma,Bulaga Sande amesema benki hiyo imekuwa ikitoa huduma za
kuwafungulia akauti maalumu bure wajasiliamali hasa kwa wanawake ambapo
kwa siku nane wameweza kuwafungulia
wanawake zaidi ya akauti 1000 benki katika maonesho ya viwanda yaliyofanyika Mkoa wa Kigoma.
Sande amasema kuwa wameona jambo jema kuwapatia fursa za kibenkj wanawake wakati ambao wanaendelea kufanya biashara hasa ya utunzaji wa fedha zao,fursa ya kupatiwa mikopo pamoja na kutoa elimu ya kifedha.
Rebeca Paul, Mfanyabiashara
na Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa Manispaa ya Mpanda amewaomba wanawake kuchangamkia
fursa za kufanya biashara hasa kuondoa hofu na kuwa na usubutu.
Amesema kutokana na
mwanamke kuwa na majukumu mengi kwenye familia bado anayofursa ya kufanya
biashara kupitia teknolojia ya mitandao yaani Online ambapo atakuwa na uwezo wa
kufanya biashara akiwa nyumbani.