Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akizungumza na wananchi wa Kata ya kasokola katika mkutano wa hadhara. |
Na Paul Mathias,Mpanda.
Serikali katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imesema haitasita kuchukua sheria kali kwa walewote watakaobainika kuavamia maeneo ya vyanzo vya maji na kuyafanyia shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji.
wananchi wa Kata ya Kasokola wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph kwenye mkutano wa hadhara kijijini hapo. |
Serikali katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imesema haitasita kuchukua sheria kali kwa walewote watakaobainika kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji na kuyafanyia shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji.
Onyo hilo limetolewa na mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph
wakati akizungumnza na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Kata ya Kasokola Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi.
Amesema kuwa kuna taarifa kwa baaddhi ya wananchi katika Kijiji
hicho wameanza kufanya kazi za kilimo na ufugaji katika chanzo cha Maji Manga
ambacho ni chanzo kikubwa cha maji katika Manispaa ya Mpanda na kuwataka
kuondoka mara moja kwenye chanzo hicho cha maji.
Diwani wa Kata ya Kasokola Chrisant Mwanawima akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara baina ya mkuu wa Wilaya na wanachi wa Kasokola |
Amessitiza kuwa serikali haitakuwa na msaliamtume kwa yeyote
atakae bainika kunfanya kazi katika chanzo cha Maji Manga kwakuwa chanzo hicho
nitegemeo kubwa katika mradi wa maji wa Miji 28 ambao utakuwa muarobaini wa
upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Mpanda.
Waliovamia kwenye chanzo hiki cha Manga watupishe haraka kwani chanzo hiki ni mhimu sana kwakuwa utasaidia
upatikajaji wa Maji kuptia mradi wa Miji 28 kutokea bwawa la milala ambao
unatekelezwa kwa zaidi ya Bilioni 22 amesema Jamila yusuph Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda.
Wananchi wa Kata ya Kasokola wakiwa katika utulivu wakati wa mkutano huo baina yao na mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph |
‘’watu wa Bonde mnakisimamia hiki chanzo wananchi wamesema hapa
chanzo kimevamiwa kuna watu wanakata mkaa mifugo inangia kule nanyie watu wa
Bonde nawapa siku saba mnipe taarifa mmefanya nini juu ya uharibifu huu
ulioelezwa wa chanzo hicho cha Maji amesema mkuu huyo wa Wilaya ya Mpanda
Jamila yusuph.
Paul Ilesha mkazi wa Kijiji cha Kasokola amesema amemshuru mkuu
wa wilaya kwa kuja na kutoa maagizo kwa wale waliovamia chanzo cha Maji Manga
waondoke.
Thadeus Ndeseiyo afisa maendeleo ya Jamii kutoka Bodi ya Maji Bonde la Mto Ziwa Rukwa akitoa elimu kwa wananchi wa Kasokola juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya Maji |
Kwa upande wake Afisa maendeleo kutoka bonde Ziwa Thadeus
Ndeseiyo amewaomba wananchi hao kuwa walinzi wa chanzo hicho cha Maji kwakuwa
maji ni uhai.
Ndeseiyo anasema ‘’Ukikiingilia tu hiki kidaka maji cha Manga
vilevisima tulivyo chimbiwa na serikali vinakauka kwahiyo tunapovamia chanzo
hiki tutakosa maji lazima kila mtu awe mlinzi wa mwenzake kukilinda na kutoa
taarifa za uhalibifu wa chanzo hiki.
wananchi wa Kasokola wakiwa katika mkutano wa hadhara baina yao na mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila yusuph |
kwahabari zaidi endelea tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com