CRDB BENKI YATOA MADAWATI 162 KUSAIDIA ELIMU KATAVI

 

Meneja wa Benki ya CRDB Mpanda Hamad Masoud[ Kushoto ]akimkabidhi Madawati Afisa elimu Sekondari Manispaa ya Mpanda Afred Kimeme[Kushoto] Pamoja na Emanuel Biganio Afisa uhusiano na Biashara CRDB Benki Kanda Mbeya [Kulia ] akiwa kabidhi madawati wanafunzi wa Sekondari Kawalyowa

Na Paul Mathias, Katavi

Benki ya CRDB Tawi la Mpanda Mkoa wa Katavi imetoa Madawati 162 kwa Shule Tatu za sekondari ili kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa za serikali katika kuimarisha miundo mbinu ya Elimu katika mkoa wa Katavi na Tanzaniakwa ujumla.

Wanafunzi wa  Sekondari Kawalyowa wakiwa wameketi kwenye Madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB Shuleni Hapo.

Benki ya CRDB Tawi la Mpanda Mkoa wa Katavi imetoa Madawati 162 kwa Shule Tatu  za sekondari ili kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa za serikali katika kuimarisha miundo mbinu ya Elimu katika mkoa wa Katavi na Tanzaniakwa ujumla.

Akikabidhi Madawati hayo Katika shule ya Sekondari Kawalyowa na Maluja Sekondari zilizopo Manispaa ya Mpanda pamoja na Sekondari ya Majalila iliyopo Wilaya ya Tanganyika Meneja wa Benki ya CRDB Hamad Masoud amesema Benki hiyo inatoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kurejesha wanachokipata kupitia wateja wao.

‘’Benki yetu ya CRDB katika jitihada zake za kusaidia sekta ya Elimu Katika Mkoa wa Katavi tumetoa msaada wa Madawati 162 Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Tanganyika na tutakwenda Hadi Halmashauri ya Mpibwe madawati haya kwa ujumla wake yanathamani zaidi ya  Shilingi Milioni 7 ‘’amesema Masoud

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mpanda Hamad Masoud akimkabidhi Madawati Diwani wa Kata ya Kakese Maganga Salaganda katika Shule ya Sekondari Maluja iliyopo Kata ya Kakese.

Amesema katika Msaada huo Shule ya Sekondari Kawalyowa imepata madawati 40 huku Shule ya Sekondari Maluja ikipatiwa Madawati 32 na Shule ya Sekondari Majalila ikipatiwa Madawati 40 huku Madawati 50 yatakwenda kukabidhiwa Halmashauri ya Mpibwe.

Kwa upande Emanueli Biganio Afisa mahusiano Biashara na serikali kutoka CRDB Benki kanda ya Mbeya amesema Benki hiyo imekuja na Kampeni maalumu inayojulikana kama Keti Jifunze ambao utatekelezwa ambao utatekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

‘’Juhudi hizi za kuunga mkono Elimu tunaufanya nchi nzima sio tu hapa Katavi ila nchi nzima mpango huu tumeupa jina la Keti Jifunze tunataka watoto wakae na wasome kama vile ambayo Serikali inasisitiza na kuendelea Kuboresha Miundo mbinu ya Elimu’’ amesema Biganio.

Muonekano wa Shule ya Sekondari Maluja iliyopo Kata ya Kakese Manispaa ya Mpanda ambayo imepatiwa Madawati Kutoka Benki ya CRDB Benki

Fred Kimeme Afisa elimu Sekondari Manispaa ya Mpanda wakati akipokea Madawati hayo ameishukuru Benki ya CRDB Kutoa msaada huo wa Madawati kama sehemu ya kusaidia Sekta ya Elimu ksatika manispaa ya Mpanda.

‘’niwapongeze CRDB kwa Msaada huu sisi wasimamizi wa Elimu tunaimani hiki walichokitoa kitawasaidia wanafunzi hawa kukaa na kusoma kwa utulivu amesema’’ Kimeme

Salome antony Mwanafunzi wa Sekondari Kawalyowa ameishukuru Benki ya CRDB Benki kwa kuwaletea Madawati hayo watayatumia vizuri katika kujifunza na kuongeza maarifa katika kutimiza ndoto zao kielimu.

Meneja wa CRDB Benki Tawi la Mpanda Hamad Masoud akimkabidhi Dawati Mkuu wa Shule ya Sekondari Majalila 

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kakese Maganga Salaganda pamoja na Diwani Kata ya Ilembo Joseph Kang’ombe wamesema Benki ya CRDB inachokifanya ni sehemu ya kutekeleza uimarishaji wa Elimu kwa vitendo ikiwa ni sehemu ya Kuisadia serikali katika kuimalisha huduma za Elimu katika Manispaa ya Mpanda.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages