![]() |
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupatiwa
huduma na madaktari bingwa Bobezi wa kutoka katika Hospitali
ya Rufaa ya Benjamini Mkapa wakiwa katika hospital ya Rufaa ya
Mkoa wa Katavi |
Na Walter Mguluchuma,Katavi
zaidi ya Wananchi 1000 wamejitokeza kwa muda wa siku tano kuweza kupatiwa matibabu mbalimbali yaliyotolewa na madakitari Bingwa wabobezi wa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa huku mwikio wa wananchi waliofika kupatiwa huduma hizo ukiwa ni mkubwa
![]() |
Mkuu wa Kitengo
cha mawasiliano na mahusiano wa Hospitali
ya Rufaa ya Benjamini Mkapa Jeremia Mbwambo
akielezea namna ambavyo madakitari bingwa
bobezi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa
walivyoweza kufanya kazi za kuwahudumia wananchi mpaka muda
usiku wa manane pasipo kuchoka
|
zaidi ya Wananchi 1000 wamejitokeza kwa muda wa siku tano kuweza kupatiwa matibabu mbalimbali yaliyotolewa na madakitari Bingwa wabobezi wa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa huku mwikio wa wananchi waliofika kupatiwa huduma hizo ukiwa ni mkubwa
Daktari Kiongozi anae husika na usimamizi wa utowaji wa huduma bora katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt Parason Mtasingwa alisema wamepokea madakitari Bingwa wabobezi 12 kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa toka tarehe 11 mwezi huu hadi tarehe 15 mwezi huu walipohitimisha utowaji wa huduma hizo wakiwa wameshirikiana na madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi .
Mwitikio wa wananchi umekuwa ni mkubwa kwa sababu
wako juu sana malengo ya wagonjwa waliokuwa wamepanga kuwahudumia kwa
muda huo wa siku tano kwani kwa muda wa siku nne
walikuwa wamewaisha wahudumia wagonjwa 879 ambao wako zaidi ya
wagonjwa waliokuwa wamepanga kuwahudumia kwa muda wa siku tano .
![]() |
Mbunge wa Viti
maalumu Mkoa wa Katavi Tasca Mbogo akielezea namna
alivyopata wazo la kuwaomba madaktari Bingwa bobezi wa
Hospitali ya Benjamini Mkapa kuja mkoani Katavi kutowa huduma
za udaktari bingwa baada ya kuona kuna mahitaji hayo na
amewahakikishia wananchi atawaomba waje tena kutona na jinsi
watu wanavyohitaji kuduma hiyo
Sambamba na hilo wapo zaidi ya wagonjwa zaidi ya mia mbili ambao wameweza kufika lakini hawakuweza kuwahudumia kutokana mwitikio huo wa watu kuwa mkubwa wagonjwa kuwa wengi na ufupi wa muda wa siku za zilizipangwa kutowa huduma .
Alisema kwa ujumla zoezi hilo limekwenda vizuri kwa
watuwalipatiwa huduma kwani wagonjwa waliofika wameweza kapatiwa
huduma za vipimo upasuaji ,dawa na ushauri kuhusu
afya zao na kwa wagonjwa walionekana na matatizo
makubwa hasa ya upasuaji umewekwa utaratibu mzuri wa
kuweza kuwafuata huko huko madakitari bingwa hao ili
wakaweze kufanyiwa upasuaji mkubwa katika Hospitali ya Benjamini
Mkapa .
Dkt Mtasingwa amemshukuru Rais
Dakta Samia Suluhu Hassani na Wizara ya
Afya kwa kuweza kuwajengea uwezo wa udaktari Bingwa na
ubobezi kwa hao madaktari na pia
kuweza kuziwezesha taasisi mbalimbali zinazotowa
huduma kwa upande wa afya .
Amebainisha kuwa kwa muda huo wa siku tano
madakitari bingwa wabobezi hao wameweza kufanya
opesheni 49 za magonjwa mbalimbali na bado walikuwa wakiendelea
na upasuaji mwingine kwenye
siku ya tano ya kumalizia kutowa
huduma kwenye Hospitali hiyo ya Katavi .
Alifafanua kuwa idara ya magonjwa ya akina mama
na uzazi . watoto mifupa na magonjwa ya ndani yamekuwa
na mwitikio mkubwa sana wa magonjwa pia wamemshukuru Mbunge
wa Viti Maalumu Tasca Mbogo kwani amekuwa
karibu sana na madaktari hao kwa muda wa siku zote tano amekuwa akiwapa
ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha huduma zinatolewa kwa
wananchi kwa jinsi ilivyokusudiwa .
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi Tasca Mbogo
amesema watu wamejitokeza kwawingi kwani ukiangalia jiografia ya Mkoa wa Katavi
mtu anapokuwa amepewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Kanda kwa ajiri
ya kupatiwa matibabu ulazimika kusafiri umbali wa
kilometa mia nane hivyo ndio maana wamejitokeza kwa wingi kutokana
na huduma hiyo ya kibingwa kusogezwa karibu .
Mbogo alieleza kuwa kutokana na mahitaji ya watu wa Mkoa
wa Katavi kuhitaji huduma za madaktari bingwa bobezi ndio
maana yeye alipata wazo la kuomba Madaktari
bingwa bobezi kutoka katika hospitali ya Benjamini
Mkapa waweze kufika katika hospitali ya Mkoa wa Katavi .
Kwanza alimshukuru Rais Dkt Samia
kwa kujali afya za Watanzania na kwa ujenzi wa
Hospitali za Rufaa za mikoa na vituo vya afya katika ujenzi huo
mafanikio hayo yameweza kusaidia mkoa wa Katavi kwa kuweza
kuwa na hospitali ya Mkoa yenye madaktari bingwa na vifaa vya kutosha na
ndio maana madaktari wa Benjamini Mkapa wameweza
kufanya kazi bila shida kwani wamekuta kuna vifaa vya kutosha
na vya kisasa .
Alisema kutokana na hali ya mwitikio kuwa mkubwa
amewaomba madaktari bingwa wa Benjamini Mkapa
wasimchoke kwani atawaomba tena kama alivyowaomba wakati huu
waje tena Mkoani Katavi kuwahudumia wananchi kwa
kuwapatia matibabu na ushauri kwani imeshindikana kuwahudumia wananchi
wote waliotijaji kutokana mwitikio kuwa mkubwa na muda kuwa
mchache .
Taska Mbogo amewahakikishia wananchi wa
Mkoa wa Katavi kuwa ajitahidi kadri ya
uwezo wake madakitari hao warudi tena katika Mkoa wa Katavi
ili waweze kutowa tena huduma hiyo kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi
Nae Jeremia Mbwambo mkuu wa kitengo cha
mawasiliano na mahusiano wa hospitali ya
Benjamini Mkapa alisema lengo la madaktari wa
hospitali hiyo ilikuwa ni kuhudumia watu 400 hado 500 wameweza kufika
watu zaidi ya 1000 waliohudumiwa ni 879 hivyo wamelazimika kutowa huduma wakati
mwingine hadi usiku wa manane hasa kwenye kufanya upasuaji .
Hali hiyo inaonyesha jinsi wadakitari hao walivyoamua
kufanya kazi za dhati za kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Katavi
na pia imeonyesha jinsi Mbunge wa viti Maalumu Tasca Mbogo
alivyowapokea tangia alivyoanza kuratibu zoezi hilo toka mwanzo .
Mwambambo amebainisha kuwa sio jambo dogo
kuleta madakitari 12 waliokuwa wameongozwa na Mkurugenzi wao
Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa maana unapowatowa kwenye
hospitali ya rufaa unaona kuna mzigo Fulani wa wananchi utakuwa umetoka
katika kuwahudumia wananchi lakini kutokana na jinsi walivyojipanga ndio
maana walikubali madakitari hao waweze kufika Katavi ni jambo la
kumshukuru Mkurugenzi wao Dkt Alfonce
Chandika kwa kuweza kuridhia
Mkazi wa Mtaa wa Mtaa wa Makanyagio Manispaa ya
Mpanda Crekensia Malango aliwashukuru Madakitari
kwa kuweza kumfanyia upasuaji mkubwa mtoto wake
aliyekuwa anatatizo la kuwa na utumbo mkubwa lakini baada ya
kufanyiwa upasuaji huo mwanae kwa sasa anaendelea vizuri huku akiwa bado
anapatiwa matibabu .