Mkurugenzi Mtendaji wa Hosptali ya Benjamin Mkapa-Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi.
Madaktari Bingwa wabobezi wa Hosipitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa wameanza kutowa huduma ya matibabu ya udaktari wa kingwa wa magonjwa mbalimbali ikiwa ni jitihada za Hospitali hiyo kuwafikishia Wanzania huduma za kiafya mahali walipo,
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko wakati akizungumza na madaktari bingwa na bingwa bobezi (Hawaonekani kwenye picha) katika ofisi yake leo. |
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Dkt Alphoce Chandika ambae ameongoza timu hiyo ya madaktari amebainisha kuwa wapo Mkoani Katavi kwa ajiri ya kutowa huduma za kiafya kwa kuwa moja ya adhima ya Serikali imeisha towa mwongozo unao wataka watoke nje ya Hospitali na kwenda kuwahudumia wananchi huko waliko na ndio maana wameamua kufika Katavi .
Mkoa wa Katavi ni moja wapo wa maeneo ambayo yamekuwa yakituma wagonjwa mbalimbali kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa kama sehemu yao ya rufaa kwa kuwa Hospitali hiyo ni moja katika ya Hospitali za Rufaa za Kanda zinazotowa huduma za kibingwa hapa nchini .
Dkt Chandika ameeleza kuwa wamekuwa kwenye Hosipali ya Benjamini Mkapa wakiwa na wataalamu waliopata ujuzi wa kidaktari ndani na je ya nchi kwa ajiri ya kuwahudumia wananchi na wameanza kutowa huduma za ubingwa bobezi ukiwemo upandikizaji wa figo na kuna maabara maalumu kwa ajiri ya magonjwa ya moyo kwa mantiki hiyo hizi huduma zinatakiwa kuwafikia wananchi hivyo wameamua kufika Katavi ili kuwahudumia wananchi pasipo wao kusafiri umbali mrefu kwenda Dodoma.
Baadhi ya Madaktari bingwa na bingwa bobezi kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma wakishuka kwenye ngazi baada ya kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi. |
Amefafanua kuwa wamekuwa wakipata wagonjwa wengi kutoka kwenye ukanda huu kwani levo ya Hosiptali ya Mkoa wa Katavi sio huduma zote za matibabu ya kidaktari bingwa zinaweza kuwa zinapatikana hivyo Serikali ya awamu ya sita imewawezesha vifaa vya kuweza kutowa huduma hiyo ya mkoba na ndio maana waweza kufika Katavi kwa kuwa patia wananchi huduma zilizoimarika mahali wanapo ishi .
Wapo Mkoani Katavi madaktari 12 wa kutoka Benjamini Mkapa ambapo watajikita zaidi kwenye utaalamu wa magonjwa kumi na moja ambapo wanae daktari bingwa wa magonjwa ya ubongo na mishipa ya fahamu kwani wamebaini kuna watotowanaotoka huku kwenda kutibiwa huko wanaozaliwa wakiwa na vichwa vikubwa hivyo wamekuja na vifaa ambavyo watawahudumia hapo hapo kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi na kuwapunguzia adha ya usafiri .
Pia wanae dkt wa magonjwa wa mfumo wa mkojo kwa kuwa tatizo hilo lipo kwa wazee,wanae pia dkt wa watoto wamebaini kuna matatizo ya watoto wanaozaliwa wakiwa na matatizo ya moyo vilevile wanamadaktari bingwa wa mifupa na viungo .
Amewataja madaktari wengine kuwa ni wamagonjwa ya kina mama na uzazi macho figo wanawashukuru Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi na Mikoa ya jirani wajitokeze kwa wingi kwani wao wamejipanga kuwahudumia wote pia mbali ya kutowa matibabu watatowa pia na ushauri kwa watu wenye magonjwa mbalimbali .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametowa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi kujitokeza kwa wingi kuweza kupatiwa huduma za madakitari bingwa hao kwani haja wahi kupokea malalamiko yoyoye ya kutoka kwa wananchi wanaokuwa wanakwenda kutibiwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa hali hiyo inaonyesha jinsi huduma zao zilizokuwa na ubora .
Amesema kuwa ni vema wananchi watumie furusa hiyo ambayo itakayokuwa inatolewa ili waweze kupatiwa huduma nzuri pamoja na ushauri anafahamu Mkoa wa Katavi unayo hospitali ya Mkoa ya Rufaa lakini haina madakitari bingwa lakini bado hawaja timiza madakitari bingwa wa kwenye vitengo vyote .
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt Damiani Maruba ameeleza kuwa ujio wa wataalamu |
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt Damiani Maruba ameelez
a kuwa ujio wa wataalamu utawasaidi wao kuweza kujiongezea utaalamu zaidi ambao hawakuwa nao awali .
Aidha amesema hospitali hiyo haina wataalamu mbalimbali kama vile wa watoto ,figo magonjwa ya ndani , mtaalamu wa magonjwa ya ufahamu mtaalamu mbobezi wa mfumo wa chakula hizo ni baadhi ambazo hawana wataalamu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.
Dkt Maruba amesema kwa timu hiyo ya madakitari inatarajiwa kufanya kazi katika Mkoa wa Katavi kwa muda wa siku tano ambao kwa siku ya kwanza wameweza kujitokeza watu zaidi ya 150