WANANCHI WASHAMBULIA GARI LA KAIMU RPC KATAVI NA KUHARIBU NYUMBA YA DIWANI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani

Na Walter Mguluchuma,Katavi

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi katika Kijiji cha Ikola Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wameharibu Nyumba ya Diwani wa Kata ya Ikola Philmoni Molo pamoja na Nyumba ya kulala wageni ya Mfanyabiashara mmoja aliejulikana kwa Jina la Ogoza wakiwa tuhumu kwa kutoa taarifa Polisi ili kuzuia zoezi la kuwatambua wachawi linalofanywa na watu maalufu kwa majina ya Kamchape.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi katika Kijiji cha Ikola Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wameharibu Nyumba ya Diwani wa Kata ya Ikola Philmoni Molo pamoja na Nyumba ya kulala wageni ya Mfanyabiashara mmoja aliejulikana kwa Jina la Ogoza wakiwa tuhumu kwa kutoa taarifa Polisi ili kuzuia zoezi la kuwatambua wachawi linalofanywa na watu maalufu kwa majina ya Kamchape

Kwa mujibu wa Mashuhuda wa tukio ambao hawakuwa tayari Kutajwa Majina yao wamesema kuwa tukio hilo limetokea leo mchana wakati wakati wa tukio hilo Asikari Polisi waliokuwa wakioongozwa na Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Agust Urio  licha ya kutaka kuwatawanya Wananchi waliokuwa na Silaha za jadi walifanya Mashambulizi ya kuwashambulia Polisi huku polisi wakiwatawanya Wananchi anbao hawakuwa tayari kutii na waliendelea kuwashambulia polisi na kuharibu Mali za Mfanyabiashara huyo.

Kabla ya kufanya Tukio hilo kundi hilo la wananchi ambalo wengi wao ni Vijana Wakiwa na Kamchape  walifika Nyumbani kwa Diwani walimkuta mkewe ndipo walipoanza kushambulia Nyumba hiyo kwa Kuvunja vioo vya Nyumba hiyo na kuchukua Vitu Mbalimbali ikiwemo Cleti za Soda na Bia.

Wananchi hao waliaendelea kupiga Makelele wakidai kuwa Diwani huyo ametoa taarifa kwa Jeshi la polisi juu ya uwepo wa zoezi la kuwabaini wachawi kijijini hapo ambalo linafanywa na watu wanaojiita Kamchape.

Wakati wananchi hao wakiendelea kufanya Uharibifu huo Jeshi la Polisi lilitumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya Wananchi hao lakini wananchi hao waliendelea kufanya uharibifu huo huku wakiwashambulia Polisi kwa silaha za jadi na kuwarushia Mawe polisi ili waondoke eneo hilo kwakuwa wananchi hao wamechoshwa na Vitendo vya Kishirikina kijijini hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesemo Buswelu amekiri kupokea kwa Taarifa hizo na kuahidi kesho kufika katika Kijiji cha Ikola ili kufatilia swala hilo kiundani zaidi.

‘’nimepata taarifa hizo na kesho asubuhi naenda huko’’ amesema Mkuu  huyo wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu wakati akiongea na Mwandishi wa Chombo hiki kwa njia ya Simu.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Agust Urio alipotafutwa kwanjia ya Simu kuzungumzia suala hilo amesema amesekia tukio hilo na kesho atalifatilia na kutoa taarifa zaidi.

''hata mimi nasikia tu kuwa kunatukio la nyumba ya Diwani kuharibiwa kesho nitafatilia amesema Kaimu kamanda Huyo Agust Urio

Mnamo Tarehe 29/8/2023 chombo hiki kiliandika habari juu ya taarifa za wananchi wa Tarafa ya Karema kuchangishana Pesa kwaajili ya kuwalipa Waganga wa Kienyeji Maalufu Kamchape iliwafike eneo hilo kuwabaini Wachawi

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages