DC MLELE VIONGOZI WA SERIKALI TUMIENI SHERIA UHIFADHI WA MISITU.

 

Mkuu wa wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Majid Mwanga akikagua baadhi ya bidhaa zilizozalishwa na wajasiliamali  ambapo zimewekwa kwenye maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi.

Na George Mwigulu,Katavi.

Watumishi wa serikali ambao wamepewa dhamana ya kusimamia uhifadhi wa misitu na mazingira pamoja na watendaji wa kijiji na kata wametakiwa kutumia sheria kwa ajili ya kuhakikisha hakuna mtu anayekata miti bila kibali kutoka kwa mamlaka husika za serikali.

Ukataji miti kiholela umekuwa tishio kubwa la uharibifu wa mazingira katika Mkoa wa Katavi jambo ambalo ni chanzo cha joto na ukame kuanza kuunyemelea mkoa huo.

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,Majid Mwanga katika viwanja vya CCM Azimio Manispaa ya Mpanda kwenye wiki ya Mwanakatavi ambapo ilikuwa ni sehemu ya Utalii na Uhifadhi wa Mazingira.

Mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa kitendo cha ukataji miti unapaswa kudhibitiwa kwa haraka zaidi ili kulinda uoto wa asili ambao umekuwa chanzo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Katavi kupitia ufugaji wa nyuki na mvua ambayo husaidia kwenye sekta ya kilimo.

"Juu ya uhifadhi misitu na mazingira mnafahamu mkoa wa Katavi umezungukwa na misitu ambayo ni chanzo kikubwa cha mvua na wapo wananchi wengi walio jiingiza kwenye ufugaji wa nyuki katika misitu ya asili" amesema.

Mwanga amesema kuwa jamii inapaswa kuendelea kuhakikisha kwamba uchumi unakua kupitia uhifadhi wa mazingira na misitu ya asili ambayo wametunukiwa na Mungu na serikali kuzipatia mamlaka ya TFS,Halmashauri na serikali ya kijijj kila mmoja amepewa dhamana ya kuitunza.

Ametoa tahadhari kwa wageni kutoka nje ya mkoa wa Katavi kuwa sehemu ya utunzaji wa misitu na mazingira na kuepuka kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira kupitia ukataji miti kwa sababu ya upanuzi huo wa makazi na mashaba.

Katika mikakati ya uhifadhi ya misitu na mazingira amasema kuwa serikali ya mkoa wa Katavi itaendelea kuimarisha upandaji miti na usimamizi ambayo ni Mil 1.5 hupandwa kila mwaka pamoja na taasisi za Amcos ambazo zinalima zao la tumbaku zinapaswa kuendelea kupanda miti.

Katika sekta ya utalii Mwanga amesema kuwa utalii umeongezeka kwa kasi ambapo wageni kutoka nje na ndani ya mkoa wa Katavi na wilaya zake wamekuwa wakitembelea vivutio hivyo ambapo Waziri Mkuu Msitaafu Mizengo Pinda ameongoza timu ya Mkoa kwenda kutalii katika hifadhi ya taifa ya Katavi.

Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Katavi,Shija Zengo ameishukuru serikali ya mkoa wa Katavi kupitia maonesho ya wiki ya Mwanakatavi wamehamasika kulinda misitu baada ya kupata elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

Shija anasema kuwa moja ya elimu aliyoipata ni athari ya uvamiaji wa misitu kwani kuvamia misitu huongeza shughuli za binadamu ambazo zinaweza kuathiri upatikanaji wa asili bora.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages