MAANDALIZI WIKI YA MWANAKATAVI YAMEKAMILIKA

 

Neemia James Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Mwanakayavi itakayoanza October 25/31 katika Viwanja vya CCM Azimio Mpanda Mjini.

Na Paul Mathias-Katavi

Ikiwa imebaki siku moja kuanza kwa wiki ya Mwakatavi ambayo itazinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kuanzia 25/10/2023 hadi 31/10 2023 katika Uwanja wa CCM Azimio Mpanda Mjini.

Muonekano wa Mabanda kuelekea Wiki ya Mwanakatavi Katika Viwanja vya CCM Azimio  

Ikiwa imebaki siku moja kuanza kwa wiki ya Mwakatavi ambayo itazinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kuanzia 25/10/2023 hadi 31/10 2023 katika Uwanja wa CCM Azimio Mpanda Mjini.

Tumefika katika Viwanja vya CCM Azimio ili kjionea maandalizi yanavyoenenda kufikia wiki ya Mwanakatavi ambapo tumeona maandalizi yakiwa yanaelendelea huku tukishuhudia taasisi mbalimbali zikiendelea kuweka mabanda kwaajili ya shughuli hiyo.

Neemia James Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Mwanakatavi amesema kuwa maandalizi yamekamilika na wadau mbalimbali wakiwa wanaendelea na maandalizi ya hatua ya Mwisho kwa lengo la kuhakikisha siku hiyo inafana.

Amesema kuwa tayari wajasiliamali kutoka mikoa ya Dar es salamu na Tabora kwaajili ya kushikriki kwenye Wiki ya Mwanakatavi na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa Wingi ili kujionea bidhaa mbalimbali zonazopatikana katika mkoa wa Katavi pamoja na fursa zilizopo.

Katika hatua nyingine Neemia amebainishakuwa katika suala la utalii tayari wanyama mbalimbali wakiwemo Simba,Ngamia,Fisi na Wanyama wengine wamesha fika viwanjani hapo kwaajili ya siku hiyo kwa lengo la kutangaza utalii uliopo mkoa wa Katavi.

Wiki ya mwanakatavi inabeba dhima ya kutangaza mkoa wa Katavi katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Uwekezaji,Utalii,Michezo na  kiashiria cha kuanza kwa Msimu wa kilimo 2023/2024.

Mgeni Rasimi katika Ufunguzi wa Wiki ya Mwanakatakavi anatarajia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko na Wiki hii ya mwanakatavi itaenda Sambamba na Kaulimbiu isemayo Katavi yetu: Talii,Wekeza,Imarisha Uchumi kwa Maendeleo Endelevu.

Fursa hii ni Mhimu kwa wananchi katika mkoa wa Katavi wananchi tujitokeze kwa wingi kushiriki Wiki ya Mwanakatavi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages