Mwenekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Charles Halawa akizungumnza na wajumbe wa kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Nsimbo. |
Na Paul Mathias,Nsimbo
Baraza la madiwani katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi mkoa wa Katavi wameishauri Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini [RUWASA] kuwa na utaratibu wa kuthibiti Mapato yanayokusanywa na jumuiya za watumia maji vijijini ili kuendeleza miradi mingine.
Baraza la madiwani katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi mkoa wa Katavi wameishauri Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini [RUWASA] kuwa na utaratibu wa kuthibiti Mapato yanayokusanywa na jumuiya za watumia maji vijijini ili kuendeleza miradi mingine.Madiwani katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wakiwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani
Hoja hiyo imebuliwa na Madiwani hao katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kinajadili taarifa za taasisi naza Kata kwenye Halmashauri hiyo.
Akichangia hoja ya taarifa ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa Wilaya ya Mpanda Diwani wa
kata ya Machimboni Raphael Kalinga amesema kuwa jumuiya za watuamiaji katika
kata yake imekuwa ikikusanya mapato mengi ila changamoto ya Matumizi ya fedha
hizo imekuwa na ukakasi.
Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mpanda Mhandisi Christian Mpena akitoa taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maji Halmashauri ya Nsimbo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani |
Amesema kuwa jumuiya hizo
zikisimamiwa vizuri katika ukusanyaji wa Mapato utaisadia serikali kupata mapato
na kujiendesha kwa vyombo hivyo Vijijini.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya
Mtapenda Elieza Fyula ameishukuru Ruwasa kwa kundelea kutekekeleza miradi Maji
vijijini na kuwaomba Ruwasa kuendelea kusambaza Maji katika maeneo ya Taasisi
mpya za serikali ili wananchi waendelee kupata huduma bila usumbufu.
‘’Shule mbalimbali zinazoanshwa
kwenye Halmashauri yetu ikiwemo shule ya Msingi Shelesi na shule mbalimbali
zilizoanzishwa niwaombe Ruwasa muangalie Bajeti muone uwezekano wa kuchimba
visima vya maji ili wanafunzi na walimu waliopo katika taasisi hizo waweze
kutumia maji hayo’’ amesema Fyula
Christian Mpena Meneja wa Ruwasa
wilaya ya Mpanda akiwasailisha taarifayake kwenye Baraza hilo amesema kuwa kwa
mwaka wa fedha 2023/2024 Ruwasa katika halmashauri ya Nsimbo itakwenda kujenga
mradi wa Maji katika kijiji cha Kabuga na Bulembo wenye Ghara ya zaidi ya
Bilioni moja .
Mpena amesema kuwa watakwenda
kutekeleza mradi wa kubadilisha Pampu za mkono kwenye kwenye visima kijiji cha
masewela,Filimule' Kabulonge, Kapunga, Katumba ,Kapalala na kijijji cha Kabatini.
‘’Ripoti ya CAG inaonesha kuna
baadhi ya Vyombo wametumia Pesa Mbichi kwa hiyo serikali inakuja na mfumo mpya
wa Makusanyo ya fedha kwa njia ya mtandao BLT watalamu wa B.OT wanakuja wiki
ijayo kwaajili ya mafunzo ya GEPG kwahiyo wananchi wote watakuwa wanalipia maji
kwa njia ya Control Number ukilipa kwa Control namba fedha inaingia moja kwa
moja Benki kuu anasema Mpena ‘
Mohamed Ramadhani Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbo ameomba Mfumo wa kununua maji kwa njia ya
Luku ufungwe kwenye taasisi za serikali ili kuepusha malimbikizo ya Bili za
maji ambazo zimekuwa zinajitokeza kwenye taasisi hizo.
Charles halawa mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ameipongeza Ruwasa kwa kuendelea kutekeleza miradi ya Maji kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo ili wananchi hususani akina mama waondokane kutumia muda mwingi kutafuta maji.