WATUHUMIWA 196 KATAVI MBARONI KWA MAKOSA MBALIMBALI

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani akitoa taarifa ya matukio mbalimbali kwa waandishi wa Habari wa mkoa wa Katavi.[Picha na Paul Mathias]


Na Paul Mathias ,Katavi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikiria watu kumi na tatu kwa tuhuma za  kujihusisha na matukio ya mauaji katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo wakiwa na silaha wanazotumia kutekeleza  uhalifu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akionyesha Silaha aina ya Gobole ambalo linadhaniwa kutumika katika vitendo vya mauaji [Picha na Paul Mathias]

Jeshi la PolisiMkoa wa Katavi linawashikiria watu kumi na tatu kwa tuhuma za  kujihusisha na matukio ya mauaji katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo wakiwa na silaha wanazotumia kutekeleza  uhalifu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa mkoa wa Katavi ,ACP Kaster Ngonyani Akitoa taarifa kwa wanahabari amesema kwenye msako uliofanyika kwa kipindi cha Mwenzi Oktoba,2023 wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 196 wa makosa mbalimbali kati yao 13 kwa matukio ya mauaji.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akionesha nyara za serikali zilizokamakatwa na jeshi la Polisi mkoa wa katavi[Picha na Paul Mathias]


Kaster ameeleza kuwa watuhumiwa hao walikutwa na vielelezo ambavyo ni nondo vipande viwili, panga, marungu pamoja na bajaji moja aina ya TVS yenye namba ya usajili MC 643 DCE wanayotumia kwa ajili ya usafiri kutoka eneo la tukio  mara baada ya kumaliza kutenda uhalifu " Watuhumiwa hawa bado wanaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamaji kujibu tuhuma" Amesema.

Vilevile Jeshi hilo linawashikiria watuhumiwa 11 wakiwa na madawa ya kulevya  zinazodhaniwa kuwa ni bangi kiasi cha kete 43 sawa na gramu 22, Watuhumiwa 9 wakiwa na nyara za serikali jino moja na vipande vinne vya mnyama pori aina ya tembo pamoja na watu 12 wamekamatwa wakiwa na lita 420 za pombe haramu ya moshi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akionesha bidhaa mbalmbali zilizokamatwa na Jeshi hilo kwa watuhumiwa mbalimbali.[Picha na Paul Mathias]


Kamanda huyo amesema watu 158  wamekamatwa kwa kujihusisha na matukio ya wizi, unyang'anyi, uporaji, uvunjaji, uzembe na uzururaji ambapo wamekutwa wakiwa na mali za wizi baadhi yake ni pikipiki moja aina ya Sang Lg namba MC 695 BPU,Laptop mbili,Radio sabufa sita na shata za alminiam bando tatu.

" Baada ya zoezi la usalimishaji silaha haramu kwa hiari kumalizika tumeanza kufanya misako kwa wale waliokaidi kuzisalimisha kwa hiari na tumefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja na silaha aina ya gobore" Amesema.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akionyesha moja ya silaha zinazotumiwa na waharifu kufanya Matukio ya uharifu.[Picha na Paul Mathias]

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwafikisha watuhumiwa 148 wamefikishwa mahakamani ambapo watuhimiwa 74 wamehukumiwa vifungo gerezani,watuhumiwa 22 wamehukumiwa kulipa faini,Watuhumiwa 6 wameachiwa huru na 46 bado kes zinaendelea mahakamani.

Aidha Kaster amewashukuru wananchi kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika nyanja mbalimbali katika kukabiliana na uhalifu kwani uhalifu hauvumiliki kwa sababu unarudisha nyuma maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages