Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Katavi Mhandisi Peter Ngunula akifunga Mafunzo kwa watoa huduma ngazi ya jamii CBWOSS zipatazo 22 katika mkoa wa Katavi yaliyodumu kwa muda wa siku 10 |
Wakala wa Maji
na Usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa Mkoa wa Katavi inatalajia kuongeza
ukusanyaji wa Mapato kupitia huduma ya utoaji wa Maji vujijini baada ya kuanza
kutumia Mpya wa malipo ya Huduma ya Maji kwanjia mtandao uliounganishwa na
Mfumo wa Malipo ya Serikali GPG.
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa Mkoa wa Katavi inatalajia kuongeza ukusanyaji wa Mapato kupitia huduma ya utoaji wa Maji vujijini baada ya kuanza kutumia Mpya wa malipo ya Huduma ya Maji kwanjia mtandao uliounganishwa na Mfumo wa Malipo ya Serikali GPG.
Akizungimnza
wakati akifunga Semina ya Siku kumi kwa viongozi wa utoaji wa huduma ya Maji
ngazi jamii CBWOSS Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Katavi Mhandisi Peter Ngunula
amesema kuwa mfumo huo utasaidia katika ukusanyaji mapato kwakuwa wateja
watalipia bili zao za huduma ya Maji kwa njia ya simu na fedha hizo kuingia
katika mfumo wa malipo ya serikali.
Ngunula amesema
kuwa Ruwasa Mkoa wa Katavi itaendelea kutoahuduma ya Maji Vijijini kwa kadri
inavyowezekana ili wananchi waendelee kupata huduma ya Maji kwa ukaribu Zaidi
kwa kuweka miundombinu rafiki kwenye makazi yao.
Amewaasa
Viongozi wa utoaji huduma ya Maji ngazi ya Jamii kwenda kufanya kazi kwa
kuzingatia weledi na uzalendo kupitia mafunzo waliyoyapata kwa kuwahudumia
wananchi pasipo na kikwazo chochote ikiwa ni sehemu ya kuiasaidia serikali
katika kuongeza Mapato kupitia Ruwasa.Washiriki wa Mafunzo hayo wakimsikiliza kwa umakini Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Katavi Mhandisi Peter Ngunula akifunga mafunzo hayo.
''JukumukubwalaMsingi ambalo mmelisema kwenye kiapo nikuhakikisha mnazingatia maadili mmekula
viapo lakini ni dhahili kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa wale wote ambao
watakwenda kinyume na viapo hivi msitumie fedha mbichi akaunti za makusanyo zipo fedha zote zipelekwe Benki amesema Mhandisi ‘’Ngunula.
Kwa upande wake
Masoud Almasi Kutoka Wizara ya Maji kitengo cha Tehama amesema kuwa katika Mkoa
wa Katavi wameweza kuziingiza katika mfumo jumla ya CBWOSS 22 kutoka wilaya
zote za Mkoa wa Katavi zikiwa na jumla ya wateja wapatao 5467.
Ameeleza kuwa
tangu waanze kutoa mafunzo hayo kwa kuzingaunisha CBWOSS katika mfumo wa malipo
ya serikali jumla katika mikoa Sita Hapa nchini jumla ya CBWOSS 183 zimefikiwa
na kuuganishwa katika Mfumo huo wa GPG na kufanya jumla ya Wateja wapatao 1,40227
waliounganishwa na Mfumo huo nchinzima.Masoud Almasi kutoka wizara ya Maji kitengo cha Tehama akitoa neno kwa washiriki wa Semina hiyo.
Amewaomba
washiriki waliopatiwa Mafunzo hayo kwenda kuongeza nguvu katika kusajili wateja
wapya kwa njia ya Mtandao watakao hitaji huduma ya Maji kwenye maeneo yao
kwakuwa tayari wameshajengewa uwezo namna ya kuwasajili wateja hao wapya kwenye
CBWOSS zao.
Beata Joseph mmoja wa Washiriki wa Mafunzo hayo amesema mkuwa wanatalajia kwenda kuongeza makusanyo kwenye CBWOSS zao kwakuwa wamepatiwa mafunzo hayo ya kuwahudumia wateja kwa njia ya Mtandao hususani katika kufanya malipo ya bili zao za Maji.
Jumla ya Mikoa Sita Hapa nchini zinazotoa huduma ya Maji Vijijini Ruwasa imeweza kuunganishwa na mfumo wa Malipo ya Serikali GPG ili kuthibiti upotevu wa Makusanyo wa Mapato hayo mikoa hiyo ni Kilimanjaro,Shinyanga, Mwanza, Katavi,Rukwa,Morogoro, na Mwanza.