RUWASA KATAVI KUANZA KUTUMIA MFUMO WA MTANDAO KULIPIA HUDUMA ZA MAJI

Viongozi wa utaoji wa huduma ya Maji Ngazi ya Jamii CBWSOS Mkoa wa Katavi wakiwa katika Mafunzo Elekezi kuhusu Mfumo wa Malipo ya Serikali GPG ambao utaanza kutumiwa na wananchi katika kulipia Bili ya Huduma za Maji  Vijijini.


 Na Paul Mathias,Katavi

Viongozi wa utoaji huduma ya Maji ngazi ya Jamii CBWSOS Katika mkoa wa Katavi wamesema serikali kuja na Mpango wa Malipo ya Serikali kwa kutumia huduma za maji Vijijini unakwenda kuongeza Mapato ya Serikali kwakuwa malipo yote ya huduma za Maji zitakuwa zinalipwa kwa njia ya Mfumo kupitia simu za Mikononi.

George Busunzu Mratibu wa Mafunzo ya Vyombo vya watumiamaji ngazi ya Jamii Ruwasa Makao makuu akizungumzia Umuhimu wa Mfumo wa malipo ya serikali katika kulipia Bili za maji kwa wateja wanao hudumiwa na Ruwasa

Viongozi wa utoaji huduma ya Maji ngazi ya Jamii CBWSOS Katika mkoa wa Katavi wamesema serikali kuja na Mpango wa Malipo ya Serikali kwa kutumia huduma za maji Vijijini unakwenda kuongeza Mapato ya Serikali kwakuwa malipo yote ya huduma za Maji zitakuwa zinalipwa kwa njia ya Mfumo kupitia simu za Mikononi.

Wakizungunza katika mafunzo elekezi ya namna ya kutumia mfumo wa malipo ya serikali kwa watumia huduma za maji vijijini wamesema kuwa wakati mwingine imekuwa vigumu kuthibiti upotevu wa malipo ya bili za Maji kwakuwa malipo mengi yalikuwa yanafanyika kwa njia ya kulipa fedha Mkononi.

Viongozi wa jumuiya za watoa huduma ya Maji ngazi ya Jamii Mkoa wa Katavi wakiwa katika mafunzo ya Mfumo wa Malipo ya Serikali ambao umeanza kutumika kwa wateja wa Ruwasa 

Jackson Jozi Msimamizi wa Huduma ya watumia maji Kata ya Mpanda Ndogo Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi amesema kuwa mfumo huo utawarahishia kukusanya mapato kwakuwa utakuwa wazi kwa watumia maji kuliupa bili zao za Maji moja kwa moja kwenye Mfumo.

‘’faida ya mfumo huu ni mfumo ambao upo wazi kiasi ambacho mteja amelipia ndio kiasi ambacho atatumia tunaishukuru serikali kwa kuuleta Mfumo huu kwenye CBWSOS anasema Jozi’’

Kwa upande wake Frank Rafaeli kiongozi wa jumuiya ya watumiamaji ameeleza kuwa mfumo wa GPG Utawasaidia wateja wao kupata Bili zao za Maji kwa wakati pamoja na malipo yote ya serikali kwenda moja kwa moja Serikalini.

Rafael ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuwaunganisha katika Malipo ya serikali hali ambayo itakwenda kupunguza upotevu wa Mapato yaliyokuwa yanapotea kupitia huduma za Maji Vijijini Ruwasa.

Kaimu Mratibu wa Ruwasa Mkoa wa Katavi,Ain Gick Shoo akielezea faida ya Mfumo wa malipo ya serikali kwa Taasisi ya Ruwasa namna utakavyoongeza Mapato kwa serikali

George Busunzu mratibu wa Mafunzo ya vyombo vya watumia maji Ngazi ya Jamii Ruwasa Makao makuu amesema kuwa mteja atalipia maji kwa kutumia Control Namba ambayo itamsdaidia kupata huduma ya Maji kwa kadri ya kiwango anachokitumia kwenye huduma ya Maji.

‘’mfumo huu unafaida kubwa sana mteja atalipia Maji kwa kutumia Control namba ambayo itasoma moja kwa moja GPG hii itasaidia kwa kiwango kikubwa ukusanyaji wa Mapato ‘’amesema Busunzu

Pamoja na hayo amesema kuwa Mfumo huo utasaidia kutambua wateja wao pamoja na Mchango wanao uchangia katika mfuko wa Serikali wa Mapato kwakuwa mfumo huo utakuwa unatambua moja kwa moja mapato yanayotokana na huduma za Maji vijijini kupitia Ruwasa.

Mhandisi Masoud Almasi kutoka Wizara maji Kitengo cha Tehama akielezea umuhimu wa Mfumo wa GPG kwa Jumuiya za watumiamaji utakavyo isadia wizara ya Maji na Ruwasa katika ukusanyaji wa Mapato kupitia Bili za Maji

Kwa upande wake Mhandisi Masoud Almasi Kutoka Wizara ya Maji kitengo cha Tehama amesema kuwa wizara ya Maji imeunda Mfumo mtandao kwa kwa taasisi husika ikiwemo Ruwasa ili kuwasaidia watumiamaji kulipia Bili za maji kwa njia ya Mtandao ambao umeunganishwa na mfumo wa Malipo ya Serikali GPG.

Aamesema mafunzo hayo yamefanyika katika Mikoa ya Rukwa, Shinyanga, Morogoro, Mwanza, Kilimanjaro,Katavi ambapo watumiaji maji Vijijini watalipia Huduma ya Maji kwa njia ya Mtandao.

Ain Gick Shoo Kaimu Mratibu wa Ruwasa Mkoa wa Katavi amesema jumuiya za watumiamaji zipatazo 26 zimepatiwa mafunzo hayo ya kulipia huduma za Maji kwa wateja wao kupitia mtandao ambao umeunganishwa na Mfumo wa Malipo ya Serikali GPG.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages