WANAFUNZI 15848 KATAVI KUANZA KIDATO CHA KWANZA 2024

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akitoa taarifa mbalimbali za Elimu katika mkoa wa Katavi kuelekea Msimu Mhula mpya wa Masomo wa Mwaka 2024

 

Na Paul Mathias-Katavi

Serikali katika Mkoa wa Katavi imesema kuwahaitamvumilia mzazi au mlezi atakakae kuwa kikwazo na kukwamisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha Kwanza mapema 2024 kutokujiunga na Masomo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akitoa taarifa mbalimbali za Elimu katika mkoa wa Katavi kuelekea Msimu Mhula mpya wa Masomo wa Mwaka 2024

Serikali katika Mkoa wa Katavi imesema kuwahaitamvumilia mzazi au mlezi atakakae kuwa kikwazo na kukwamisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha Kwanza mapema 2024 kutokujiunga na Masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati akizungumnza na waandishi wa Habari Ofisini kwakwe katika kuelekea Msimu wa Shule kufunguliwa.

Mrindoko amesema kuwa wazazi na walezi wawe mfano mzuri kwa watoto wao kwa kuhakikisha wanawaandalia miundombinu rafiki ya kuhakikisha wanalipoti shule ifikapo 8/1/2024.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akiwa katika ukaguzi wa Miundo Mbinu ya Elimu Halmashauri ya Nsimbo  Wiki hii.

‘’Mzazi yeyote atakaecheza na sheria kwa kukiuka nakutokumfisha shule mtoto aliyopangiwa hatutasita kuchukua hatua kali za Kisheria’’ amesema Mrindoko.

Amewakumbusha wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanaostahili kuandikishwa Darasa la awali na Darasa la kwanza kuwaandikisha ili wapate haki yao ya kupata Elimu.

Ameeleza kuwa mkoa wa Katavi Jumla ya Wanafunzi 15848 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa Mwaka 2024 huku miundo mbinu ya Madarasa ikiwa imekamilika kwaajili ya kuwapokea wanafunzi hao.

‘’Wanafunzi hawa 15848 tayari wameshapangiwa Shule kuanza masomo 8/1/2024, shule zitakazo husika kuwapokea wanafunzi hawa ni Jumla ya Shule 69 zilizopo Mkoa wa Katavi tupo tayari kuwapokea wanafunzi hawa'' ameeleza Mwanamvua

Amebainisha kuwa mkoa wa Katavi hauna changamoto ya upungufu wa vyumba vya Madarasa kutokana na serikali ya awamu ya Sita kuleta fedha nyingi zilizojenga miundo mbinu ya Mdarasa kwaajili ya Wanafunzi.

‘’Kwa wanafunzi hawa waliofaulu madarasa yanayohitajika 330 mpaka sasa tumefanikiwa kuwa na Madarasa 343 kwaajili ya kuwapokea wanafunzi kwa Madarasa yanayoanza kwa maana hiyo hatuna upungufu wa Madarasa kwa wanafunzi wa awali Darasa la Kwanza na Kidato cha Kwanza kwa mkoa wa Katavi ‘’amesema Mwanamvua

Mkuu huyo wa mkoa amesema kwa Kipindi cha Mwaka 2023 Mwezi wa Nne hadi Mwezi wa Kuminambili Mkoa wa Katavi umepokea fedha zaidi ya Bilioni 19.4 kwaajili ya uwezeshaji wa miundo mbinu ya Elimu ya Msingi na Sekondari kwa mkoa wa Katavi.

Kuhusu zoezi la uandikishaji wa Darasa la Kwanza na Darasa la awali mkoa wa Katavi umefanikiwa kuandikisha Watoto kwa kiwango cha Kulidhisha.

‘’kwa upande wa Darasa la awali uandikishaji tumeweza kuandikisha Jumla ya Wanafunzi 15189 sawa na asilimia 35.34 huku lengo lililikuwa kuandikisha Wanafunzi 42,974 kwa upande wa Darasa la kwanza tumeweza kuandikisha Wanafunzi 23051 sawa na asilimia 58.62  huku lengo likiwa ni kuandikisha wanafunzi 39,326 amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika hatua nyiningine amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Watendaji wengine wa serikali kuhakikisha wanaendelea kusimamia miundo mbinu ya Madarasa inayomaliziwa iweze kukamilika kwa wakati.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages