Shija Sabuni Mkazi wa Kijiji cha Kapanga akiwa katika zahanati ya Kijiji hicho alipomleta mtoto wake kwaajili ya kupatiwa huduma |
Na Mwandishi wetu-Katavi
Wananchi Kijiji cha Kapanga Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameishukuru serikali kwa kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kwa kujengewa zahanati kutokana na mapato ya ndani ya fedha za hewa ya ukaa.
Nyumba ya Mtumishi wa Afya katika kijiji cha Kapanga iliyojegwa kutokana na fedha za hewa ukaa. |
Wananchi Kijiji cha Kapanga Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameishukuru serikali kwa kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kwa kujengewa zahanati kutokana na mapato ya ndani ya fedha za hewa ya ukaa
Shija sabuni mkazi wa kijiji
hicho ameeleza kuwa kabla ya kujengwa kwa zahanati hiyo ilikuwa ianawalazimu
kusafiri umbali mrefu kwenda kupata huduma ya matibabu katika kijiji jirani cha
Katuma.
‘’Tunashukuru sana zamani
tulikuwa tunahangaika sana tunaenda Katuma sema kweli tunashukuru sana mimi
nasema asanteni sana kwa kutuletea huduma hii hapa kijijini kwetu’’-Shija.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kapanga Deus Hawazi amesema kuwa kujengwa kwa zahanati hiyo kunatokana na jitihada za utunzaji wa Mazingira kijijini hapo hali iliyopelekea kuanza kunufaika na Biashara ya Hewa ukaa.
‘’Tumenufaika sana na Uhifadhi wa
mazingira baada ya kufanya matumizi bora ya aridhi tukatenga misitu ya Kijiji
tumeweza kujipatia fedha nyingi sana kwaajili ya kuuza hewa ya ukaa iliyopelekea
kujengwa kwa zahanati hii’’-Hawazi
Hawazi ameeleza kuwa katika
kijiji hicho kuna baadhi ya wananachi wamekatiwa Bima ya Matibabu kupitia fedha
za hewa ukaa ili kulahisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi Kijijini
hapo.
Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa
ataendelea kuhamasisha wananchi kuendelea kutunza mazingira ili waendelee
kunufaika na fedha za hewa ukaa ambazo zimekuwazikiletwa kijijini hapo katika
sekta ya Afya na Elimu.
‘’Tumeanza kutoa hapa tangu
27/11/2023 tulianza na wateja wachache lakini kwa sasa hivi tumeweza
kuwahudumia zaidi ya wateja 1200 toka tuanze kutoa huduma hapa’’-Samweli
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Shabani Juma ameeleza kuwa kupitia Mapato
ya ndani yanayotokana na fedha za hewa ya ukaa halmashauri hiyo imekuwa
ikijenga Miundo mbinu ya Madarasa,Nyumba za watumishi na zahanati kwenye vijiji
8 vinavyonufaika na Biashara hiyo.
‘’Ukienda mwese Pale Lugonesi utakuta
tumejenga Zahanati na Nyumba ya Mtumishi tumejenga pia ofisi ya serikali ya Kijiji
hii yote ni miradi inayotekelezwa na fedha za mapato ya ndani kupitia biashara
ya hewa ukaa’’-Shaban
Amebainisha kuwa katika kipindi cha Malipo ya awamu ya nane na Tisa halmashauri hiyo inatarajia kupokea kiasi cha Shilingi Bilioni 14 fedha zinazotokana na hewa ya ukaa ambazo zitakwenda kujenga miradi mbalimbali katika vijiji Nane vinavyonufaika na biashara ya hewa ya ukaa.