Eneo la Mwambao wa ziwa Tanganyika Karema likionekana kujaa Maji kwenye eneo la Kingo hizo.
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha
Karema Mwambao wa ziwa Tanganyika Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wamelazimika
kukimbia kwenye makazi yao wanayoishi kwa kuhofia kusombwa na maji huku wengine
kupewa makazi ya muda kwenye Shule ya Msingi baada ya ziwaTanganyika kujaa Maji
na Kufika kwenye Makazi ya Watu.
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Karema Mwambao wa ziwa Tanganyika Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wamelazimika kukimbia kwenye makazi yao wanayoishi kwa kuhofia kusombwa na maji huku wengine kupewa makazi ya muda kwenye Shule ya Msingi baada ya ziwaTanganyika kujaa Maji na Kufika kwenye Makazi ya Watu.Eneo la Makazi ya watu Kijiji cha Karema likionekana kuzingilwa na Maji
Mwenyekiti wa Kijiji cha Karema
Sililo Mpondela amesema tukio hilo la ziwa Tanganyika kujaa Maji na kuzua
taharuki kwa wananachi wa Kijiji hicho limetokea juzi kuanzia Saa tatu Asubuhi
Hadi Saa Kumi Jioni.
Amesema siku hiyo ya tukio Mawimbi
Makubwa yaliyotokana na kujaa maji kwenye ziwa hilo kulipelekea maji kufika
hadi kwenye Makazi ya watu wanayoishi hali iliyopelekea baadhi ya Wananchi
kukimbia Nyumba zao baada ya maji kujaa kwenye Makazi yao.
Huku familia Mbili zikihamishia
Makazi yao kwenye shule ya Msingi baada ya kupewa makazi ya muda na uongozi wa
Serikali ya Kijiji baada usalama wao kuwa hatarini kutokana na hali hiyo.
Kutokana na tukio hilo waathirika wa tukio hilo wameobwa na uongozi wa serikali ya kijiji kutorudi kwenye makazi yao mpaka pale hali itakapo tengemaa huku wakihofia wananchi hao kupatwa na magojwa ya Mlipuko.