Mkuu wa Wilaya ya Tangayika Onesmo Buswelu akimtishwa ndoo ya Maji Mwananchi wa kijiji cha Mpembe |
Na walter Mguluchuma-Tanganyika
Wakala wa Maji na Usafi wa
Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Tanganyika inatarajia kutekeleza miradi minne
inatakayo wanufaisha jumla ya Wananchi 35,468 katika Vijiji
nine ambavyo havina miundombinu ya maji
itakayogharimu kiasi cha shilingi BILIONI 5.3 itakayoongeza
upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Tanganyika kutoka
asilimia 78 hadi kufikia asilimia 86.
Hayo ameyabainisha Meneja wa RUWASA Mhandisi Tiuway Ninga wakati uzinduzi wa huduma ya maji katika Kijiji cha Mpembe Kata ya Katuma ambao utawanufaisha zaidi ya watu 4000 uliogharimu kiasi cha tshs 210,422,433.
Ninga Amesema RUWASA Wilaya ya
Tanganyika katika mwaka wa fedha 2024/2025
wanatarajia kutekeleza miradi minne
ambayoitawanufaisha watu 35, 468 itakayotekelezwa
kwenye vijiji vine na kugharimu kiasi cha tshs
5,385,714,753.27.
amesema hali ya upatikaji wa
maji kwa sasa katika Wilaya ya Tanganyika ni
asilimia 78 hivyo miradi hiyo itaongeza hali ya
upatikanaji wa maji safi na salama kufikia
asilimia 86 hadi kufikia hapo mwakani .
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizindua huduma ya Maji Kijiji cha Mpembe Kata ya Katuma Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika
Mhandisi Ninga ameeleza kuwa mradi wa Maji uliozinduliwa kutowa huduma ya maji utakao wanufaisha watanchi 4000 wa Kijiji cha Mpembe amesema mradi huo umewezesha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Kijiji cha Mpembeb na kuweza kupata manufaa mbalimbali .
Ameyataja baadhi ya manufaa hayo kuwa
ni kumewapunguzia umbali mrefu na
muda wa kutafuta maji hivyo kupata muda
kufanya shughuli nyingine za kiuchumi kupata maji safi na
salama .
Manufaa mengine ya mradi huo ni
kuondokana na maradhi yatokanayo na
matumizi ya maji yasiyokuwa safi na salama na
uimarishaji wa mahudhurio yatokanayo na wanafunzi
mashuleni hasa katika shule ya Msingi Mpembe .
Mradi huo wa Maji Mpembe umegharimu kiasi cha
tshs 210,422,433 umetekelezwa na
Kampuni ya Mkandarasi Kabansora
Construction Company Limeted ya Dar es salamu
Meneja wa RUWASA Wilaya yaTanganyika Mhandisi Tiuway Ninga akitoa Taarifa ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa mgeni rasimi Mkuu wa wilaya ya Tanganyika |
Miundo mbinu ambayo imejengwa hadi sasa ni ujenzi wa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo 135,000 pamoja uzio wa kuzunguka tanki ,ujenzi wa vituo vitano vya kuchotea maji vyenye jumla ya vichocheo 10, ununuzi wa pampu na ufungaji wa nishati ya umeme wa jua .
Kwaupande wao wananchi wakijiji hicho wanazungumzia upatikanaji wa huduma ya maji Vitus Joseph ni mkazi wa Kijiji cha Mpembe amesema upatikaji
wa huduma ya maji kwenye Kijiji hicho utasaidia
kumtuoa mama ndoo kichwani na kutaondoa changamoto ya
ndoa.
Roza Mbalamwezi amesema tatizo la
kutokuwa na maji kwenye eneo hilo wanaloishi likuwa ni kero
kwenye familia nyingi kutokana na akina mama kutumia muda mrefu kwenda kutafuta
maji umbali mrefu hali iliyokuwa ikiwaletea akina mama kero kubwa kutoka
kwa waume zao walikuwa wake zao kuchelewa kurudi nyumbani .
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru amesema upatikanaji wa vyanzo vingi vya maji katika Wilaya ya Tanganyika umetokana na kazi kubwa inayofanywa katika Wilaya hiyo ya kuhakikisha mazingira yanakuwa salama muda wote .
Amesisitiza kuwa watahakikisha wanaendelea
kufanya dolia za mara kwa mara za kulinda mistu
na mtu yeyete ambae atakae kamatwa akifanya uharibifu kwenye
mistu na kwenye vyanzo vya maji hawatakuwa na huruma nae watamchukulia hatua
kali za kisheria .
Amesema wananchi wa Kijiji hicho
hawakuwa na maji kwa muda mrefu lakini serikali ya
awamu ya sita kwa kuliona hilo ndio maana imewapelekea huduma hiyo
ya maji safi na salama kwenye kijiji hicho .