Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizungunza na wananchi Kijiji cha Mpembe Kata ya Katuma. |
Na Walter Mguluchuma- Tanganyika
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewaonnya viongozi wa Vijiji kuacha tabia ya kuuza ardhi bila utaratibu kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria na taratibu na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakao bainikaikiwemo kuwafikisha Mahakamani.
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mpembe Kata ya Katuma wakimkiliza Mkuu wa Wilaya ya Tangayika Onesmo Buswelu |
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewaonnya viongozi wa Vijiji kuacha tabia ya kuuza ardhi bila utaratibu kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria na taratibu na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakao bainikaikiwemo kuwafikisha Mahakamani.
Maagizo hayo ameyatoa wakati
alipokuwa akiwahutubia wananchi wa
Kijiji cha Mpembe
Kata ya Katuma wakati wa maadhimisho
ya Wiki ya Maji iliyofanyika
kiwilaya kwenye Kijiji
hicho mara baada ya kuwa amezindua
huduma ya maji kwenye Kijiji hicho na upandaji wa miti .
DC Buswelu
amesema kumekuwa na tabia ya
badhi ya viongozi wa Serikali za
vijiji kuuza maeneo ya ardhi na
bila kufuata utaratibu na wengine wamekuwa wakiwauzia watu mpaka
maeneo ambayo yamehifadhiwa jambo
ambalo limekuwa likileta
uharibifu wa mazingira .
Amesisitiza kuwa kwa
viongozi wenye tabia hiyo wahakikishe wanaacha mara moja kuuza ardhi bila kufuata utaratibu na watakao bainika kufanya hivyo hata kuwa na huruma nao hata kidog atawachukulia hatua kama na
kuwafikisha Mahakamani .
Amesema
swala la utunzaji wa mazingira
ni la kipaumbele katika Wilaya
hiyo na ndio maana kuna
vijiji nane kwenye
Wilaya hiyo ninanufaika na
fedha za hewa ya
ukaa kikiwepo na Kijiji
hicho cha Mpembe ambacho kinatarajia hivi karibuni
kupata zaidi ya shilingi
Bilioni moja za fedha ya
ukaa.
Aidha Buswelu
amewataka viongozi wa vijiji
na kamati za shule za
Vijiji vinane ambavyo
wanafunzi wa wananufaika kupa
chakula shuleni kutokana na fedha
za hewa ya ukaa kuacha mara moja tabia ya kununua
vyakula kwa bei za juu
kwani anazo taarifa kuna
viongozi wamepanga kununua
gunia moja la
mahindi kwa bei ya tshs
100,000 wakati gunia moja kwa sasa ni tshs 30,000 kwenye baadhi ya
vijiji.
Buswelu amemuomba Mungu
amsimamie na amwongoze
na amlinde ili
aweze kuwadhibiti viongozi watao jaribu
kupandisha bei ya
vyakula vya wanafunzi shuleni .
Nae Mkazi wa
Kijiji cha Mpembe
Benjamini Masanja amesema
wanamshukuru Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan kwa kuweza kuwaletea huduma
mbalimbali kijijini hapo kama
vile huduma ya maji safi na salama ambayo hapo awali walikuwa hawana .
Hivyo kutokana
na umuhimu wa uhifadhi wa mazingira
wananchi wa Kijiji hicho
wataendelea kulinda mazingira
ili yasiweze kuharibika .