MTOTO APOTEA MPANDA MAZINGIRA YA KUTATANISHA MAMA AMLILIA.


 

Sesilia Alistede Kosongwa, Mkazi wa Mtaa wa Mji wa Zamani Manispaa ya Mpanda aomba jamii kumsaidia kumtafuta mwanaye aliye potea.



Mkazi wa Mtaa wa Mji Wazamani Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amesema mtoto wake anayefahamia kwa jina la Damiano Petro Habona mwenye umri wa miaka 11 amepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Tarehe 7 mwezi wa 9, 2024 wakati akicheza na watoto wengine.

Mamam huyo wa mtoto amesema kuwa mtoto wake huyo mwenye ulemavu wa kutokusikia alindoka nyumbani akiwa amevaa mavazi ya Tshart rangi ya Njano, Suruali rangi ya Ugolo na viatu vya rangi ya blue

Mtoto aliyepotea, Damiano Petro Habona akiwa kwenye muonekano wake kabla hajapotea

Amefafanua kuwa licha ya mtoto wake kutokuwa na uwezo wa kusikia na kuongea lakini anauwezo wa kuandika jina lake vizuri. Hivyo kwa yeyote ambaye atakuwa amemuona anaombwa kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu yake au ofisi ya kijiji/mtaa au kitongoji. 


AU UNAWEZA KUPIGA KWA SIMU NAMBA 0746910171 au 0744765898.

Tizama video hapa chini zaidi ili kumuona mama akitoa maelezo ya kutosha.



 






Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages