WANAWAKE KATAVI WAHAMASISHWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Bi.Christina Mndeme Naibu Katibu Mkuu [Mazingira ]Ofisi ya Makamu wa Rais  akizungumnza na wanawake wa Mkoa wa Katavi kwenye kongamano linalohusu nishati safi ya kupikia 
Na PaulMathias-Katavi

Wanawake Mkoa wa Katavi wameobwa kuchangamkia fursa ya nishati safi ya kupikia ili kusaidia kuzuia uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Baadhi ya Wanawake wa Mkoa wa Katavi waliojitokeza kwenye Kongamano la Matumizi ya Nishati safi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mpanda Social Hall 

Wanawake Mkoa wa Katavi wameobwa kuchangamkia fursa ya nishati safi ya kupikia ili kusaidia kuzuia uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Akizungumnza na wanawake wa Mkoa wa Katavi kwenye Kongamano la nishati safi ya kupikia Naibu Katibu Mkuu[ Mazingira]Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.Christina Mndeme amesema serikali imekuja na mkakati huo wa matumizi safi ya nishati ili kuokoa mazingira.

Ameeleza kuwa nishati safi ya kupikia ndio Suluhisho la kumtua kuni mwanamke kichwani ili kuhakikisha afya za wanawake zinaimarika na kuepuka madhara ya moja kwa moja yanayotokana na nishati chafu ya kupikia.

’Kipindi cha masika kuni au mkaa huwa zinatumia muda mrefu kuwaka unatumia saa moja na nusu kupika unapotumia kuni au mkaa kwa mwezi unatumia takribani saa saba unapotumia nishati safi ya kupikia unapotumia nishati safi ya kupikia kwa wiki utatumia saa moja  kwaajili ya kupikia’’Mndeme.

Bi.Felista Mdemu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jjinsia wanawake,na makundi maalumu akieleza manufaa ya kupikia nishati safi na salama kwenye Kongamano hilo
Amebainisha kuwa serikali kuleta mpango wa matumizi ya nishati safi na salama inalenga kutumia nishati mbadala ya Gesi na umeme kwenye matumizi ya kupikia ya kila siku.

‘’tunapozungumzia matumizi safi ya nishati tunaamaanisha utumie Gesi,umeme,na biogesi’-Mdemu

Mndeme ameeleza takribani watu Elfu 33,000 wanapoteza maisha kwa sababu ya matatizo ya mfumo wa upumuaji inayotokananna na matumizi yasiyo safi na salama ya nishati ya kupikia.

Amesema kuwa ukitumia kuni na mkaa kunauwezekano wa kupata ugojwa wa pumu salatani ya Mapafu ,Kuharibika kwa mimba na matatizo ya Mgongo.

Ameeleza madhara ya kijamii yanayotokanan na matumizi yasiyo safi ya nishati ikiwa nipamoja na ndoa kuingia katika migogoro kwa kuwa wanawake wanatumia muda mwingi kutafuta kuni.

Kwa upande wake Bi.Felista Mdemu Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu amewaomba wanawake wa Mkoa wa Katavi kuipokea falsafa ya matumizi safi ya nishati safi ya kupikia ili kuondokana na madhara yanayotokanana na matumizi yasiyo safi na salama ya kupikia.

Mdemu ameishukuru serikali ya Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuhakikisha jamii inakwenda kuingia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Fortunata Kabeja Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi akitoasalamu kwa wanawake kuhusu umuhimu wa kutumia Nishati safi ya kupikia

Amefafanua kuwa Wizara hiyo itaendelea kutoa elimu kwa wanawake kupitia makongamano mbalimbali ili kumuunga mkoa Rais Dk samia suluhu Hassan kwa vitendo kuhusu matumizi safi na salama ya nishati ya kupikia.

Nehemia James Kaimu Katibu Tawala uchumi na uzalishaji amesema serikali ya Mkoa wa Katavi imeanza kugawa Mitungi ya Gesi kwa wananchi kupitia Majukwaa mbalimbali.

Amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na uhalibifu wa mazingira.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages