Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akielezea umuhimu wa Mradi huo wa umeme kwa wananchi. |
Na Jackson Gelard-Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amemtaka mkandarasi anae tekeleza mradi wa umeme wa Rea katika vitongoji 75 kwenye Mkoa wa Katavi kuhakikisha anatoa fursa za kazi kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwananvua Mrindoko akisalimiana na Meneja wa Mradi huo Novatus Lyimo |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amemtaka mkandarasi anae tekeleza mradi wa umeme wa Rea katika vitongoji 75 kwenye Mkoa wa Katavi kuhakikisha anatoa fursa za kazi kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi
Hayo ameyabainisha wakati wa kikao kifupi cha kumpokea Mkandarasi kutoka katika kampuni ya M/s Dieynem company
Ltd yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam.
Mrindoko amewataka wananchi wa Mkoa
wa Katavi kuchangamkia fursa za kazi katika vitongoji mbalimbali vilivyopo katika
vijiji vyao ambapo mradi huo unapita sambamba
na kuunganishiwa umeme katika makaazi yao ,maeneo ya taasisi na katika viwanda vidogo na vikubwa vilivyopo
katika maeneo husika.
Kwaupande mwingine Mrindoko
amesema kuwa serikali ilikua ikiendelea kusikiliza malalamiko ya wananchi juu
ya ukosefu wa umeme katika vitongoji mbalimbali ambayo yamekuwa ya kiwasilishwa
kwa njia simu ,mikutano mbalimbali
na kwa njia ya redio na kuendelea kuyafanyia kazi ili vitongoji vyote vilivyopo
ndani ya Mkoa wa Katavi viweze kuunganishiwa umeme.
Mhandisi Gilbert Furia Meneja wa Miradi ya Rea Mkoa wa Katavi akifafanua mradi huo namna ulivyaanza kutekelezwa kwa wanananchi |
Amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya
M/S Dieynem Company Ltd kuhakikisha anatekeleza mradi huo kwa ufanisi mkubwa na
kwa kuzingatia uharaka wa kazi ili kumaliza kazi hiyo kabla ya muda wa miaka
miwili kama mkataba unavyo eleza ili wananchi waweze kunufaika na mradi huo kwa
wakati.
Mhandisi Gilbert Furia Meneja wa Miradi ya Rea Mkoa wa Katavi
amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa kilomita 150 za msongo mdogo wa umeme pamoja na ujenzi wa mashine
umba (Transfomers) 75.
Gilibert amesema mradi huo utagharimu kiasi cha shilling Bilio 9.5 za kitanzania na mkandarasi amekwisha anza kutekeleza mradi huo.
Amebainisha kuwa mradi huo
utatekelezwa katika kipindi cha miezi 24 kuanzia tarehe ya kuanza mradi ambayo
ni tarehe 3 september 2024 hadi tarehe 3
september 2026.
Novatus Lyimo meneja Mradi wa umeme kutoka kampuni ya M/S Dieynem Company Ltd amesema wamekwisha anza utekelezaji wa awali wa mradi huo kwa maana ya usanifu na ndani ya muda mfupi timu ya utekelezaji itakua tayari kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo.